24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Katibu Mkuu UN aridhishwa na ukanda wa Mashariki ya Kati 

AMMAN, Jordan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema kuna haja kuitazama Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini si kwa sababu ya maeneo yaliyo na migogoro bali pia kama ukanda ulio na fursa.

Guterres ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa Kongamano la Uchumi Duniani (WEF), kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini linalofanyika nchini  hapa  na  amesifu nchi kadhaa namna zilivyoweza kujumuisha katika katiba zao baadhi ya mahitaji ya kisiasa yanayoelezewa mitaani na kuimarisha ulinzi wa kijamii, utawala bora na haki za binadamu.

Mwaka 2011, vuguvugu la maandamano lilienea katika ukanda wa nchi za kiarabu wakati vijana waliposhinikiza juu ya mageuzi na kuwaondoa watawala wa muda mrefu. Baadhi ya vuguguvu liligeuka kuwa migogoro ya muda mrefu ikiwemo nchini Syria, Libya na Yemen.

Katika ufunguzi huo, Guterres pia aligusia hatari ya mabadiliko ya tabia nchi.

 “Ukanda huu utakabiliana na athari kubwa hususan ongezeko la ukosefu wa maji, ambao utapunguza kiwango kilichopo cha ardhi na kuongeza utegemezi wa chakula kutoka nje”, alisema Guterres.

 “Nchi kama Jordan ambayo haichangii sana katika mabadiliko ya tabia nchi haiwezi kuwa mwathirika kutokana na hoja kwamba baadhi ya nchi hazitimizi wajibu wake,”aliongeza katibu mkuu huyo.

 Awali wakati akifungua kongamano hilo Mfalme Abdullah alitoa wito kwa uwekezaji zaidi wa kigeni katika Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini, akisema uwekezaji huo unahitajika ili kutengeneza mustakabali wa baadae wa ukanda huo uliokumbwa na migogoro.

“Hali yetu ya kiuchumi inatia moyo”, alisema Abdullah, lakini akiongeza kuwa uchumi wa Jordan umekabiliwa na changamoto nyingi wakati taifa hilo lilipofanya jambo sahihi kushughulikia wakimbizi karibu milioni 1.3 kutoka Syria.

Ili kufufua uchumi wake, serikali ilichukua hatua kadhaa za kubana matumizi katika siku za hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kupunguza ruzuku katika bidhaa za msingi kama vile mikate, ili kufufua uchumi na kupunguza pengo la upungufu wa bajeti.

“Mageuzi yako mbioni ili kuunga mkono na kuboresha mazingira ya biashara”, alisema Mfalme huyo katika kongamano linalofanyika karibu na bahari iliyokufa yaani Dead Sea.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Yusuf bin Alawi bin Abdullah alisema nchi za Kiarabu zinapaswa kukomesha hofu kuhusu uwepo wa Israel inayoungwa  mkono  kisiasa, kiuchumi na kijeshi kutoka Jumuiya za Kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles