27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Katibu Mkuu NaCoNGO avuliwa nyadhfa zote akituhumiwa kwa ubadhirifu

Faraja Masinde, Dar es salaam

BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO), limemvua nafasi zote za Uongozi aliyekuwa katibu Mkuu wake , Islamil Suleiman.

Akizungumza Dar es Salaam leo Januri 25, Mwenyekiti wa NaCoNGO, Nicholaus Zacharia, amesema uamuzi huo ulifikiwa baada ya  kikao cha dharura kilichofanyika mapema leo.

Amesema hatua hiyo inatokana na matokeo ya kamati ya uchunguzi ya NaCoNGO iliyoundwa na baraza hilo Desemba 19, mwaka jana ambayo iliketi jijini Dodoma.

“Baraza limefikia uamuzi huo w akumvua nafasi zote za uongozi aaliyekuwa katibu Mkuu Suleiman, kufuatia tuhuma mbalimbali dhidi yake, ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha za NaCoNGO karibu milioni 540.

“Pamoja na kutotoa ushirikiano wakutosha kwa baraza, kamati ya uchunguzi ilimkuta, Suleiman na makosa ya kuingiza kwenye baraza wajumbe watano ambao hawakuchaguliwa kwa mujibu wa kanuni za NaCoNGO, kwa ajili ya kuwakilisha Mikoamitano,” amesema.

Amewataja, wajumbe hao waliochaguliwa na, Suleiman na mikoa waliyoelezwa kutoka kuwa ni, Remmy Nemmes (Geita), George Nyanda(Simiyu), Heiman Didas(Pwani), Bakari Salum(Tanga) na Gilbert Alex(Ruvuma).

Aidha, Zacharia amesema kuwa, mtuhumiwa alikuwa akiendesha akaunti mbili za benki ya CRDB za Sh na Dola bia ya kuwa na uelewa wala idhini  ya kamati tendaji au baraza .

“Alikuwa amemuweka mtiasaini ambaye siyo kiongozi ndani ya baraza, pamoja na kutoa vitisho kwa wawakilishi wa NGOs waliokuwa wanadai uwazi na uwajibikaji wa fedha waliotoa kwa NaCoNGO,” amesema Zacharia.

Amefafanua kuwa, kufuatiab uamuzi huo, baraza hilo limemteua, Focus Magwesela kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa NaCoNGO kuanzia jana Januri 25, hadi hapo itakapo amriwa.

“Kwakuwa baadhi ya makosa aliyokutwa nayo Suleiman yana viashiria vya jinai, tunapenda kuujulisha umma mtuhumiwa siyo kiongozi katika ngazi yoyote ndani ya baraza na hatua stahiki dhidi yake zitachukuliwa,” amesema Zacharia.

Mtuhumiwa

Akizungumzia tuhuma hizo Suleiman anayetuhumiwa kutumia nafasi yake vibaya ambapo amekanusha tuhuma hizo na kusema kuwa siyo za kweli na kwamba ni mbinu za kutaka kumchafua kwa kuwa amekuwa akihoji masuala kadhaa ndani ya baraza hilo.

“Nimezipata hizi habari, lakini hizi tuhuma siyo za kweli bali kuna kitu kimefichikia kwani mimi nimekuwa nikisimama mstari wa mbele wka ajili ya kutaka sheria ya NGOs itekelezekee, lakini baadhi ya watu haiwataki kwa kuwa itabana maslahi yao, ndiyo maana wakaunda mbinu ya kutaka kuniondoa.

“Haya mambo mengine wanayosema ni siasa tu kwnai hata hiyo kamati wanayosema kwamba ilikuwa inanichunguza haijawahi hata kuniita, hivyo naona walichokuwa wanataka kufanya wamekitekeleza,” aamesema Suleiman na kuongeza:

“Kimsingi baraza tayari limemaliza muda wake na hivyo kiutaratibu uchanguzi ulitakuwa kuwa umefanyika tangu mwezi uliopita,” amesema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles