30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 23, 2021

Katambi ataka waajiri kuwathamini wafanyakazi wao

Na Sheila Katikula, Mwanza

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Sera na Ajira, Patrobas Katambi amewataka  waajiri kuwathamini wafanyakazi wao kwa sababu hufanya kazi na kuinua uchumi wa taasisi husika  hivyo ni vyema kuona thamani na umuhimu wao na kuwapa sitahiki zao kwa wakati.

Amesema walioshikilia uchumi wa nchi ni wafanyabiashara wa kati kushuka chini, ndiyo maana serikali imeamua kuwawezesha,hivyo vijana,kina mama na baba wafanye kazi na siyo  kusubiri ajira ambazo upatikanaji wake umekuwa ni watabu.

Katambi amesema hayo leo Aprili 27, jijini Mwanza alipokuwa akizungumza na waajiri, Chama cha Wafanyakazi pamoja Wakala wa Usalama na afya mahala pa kazi (OSHA) kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahala pa kazi duniani ambayo yalianza Aprili 26, mwaka huu yakitarajiwa kufikia kilele chake Aprili 28, 2021.

“Waajiri wapo wanaowanyima haki wafanyakazi wao kujiunga na vyama vya wafanyakazi, tukiwabaini sisi tutawashughulikia, hivyo wale wote walio na madai walioumizwa na wanasumbuliwa na waajiri kupata haki yake wafike wizarani ili tuweze kutatua changamoto hiyo,”amesema Katambi.

Amesema zaidi ya wajasiriamali  600 wameshiriki kwenye maadhimisho 17 tangu yaanzishwe nchini kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wamepewa mafunzo ya Usalama na Afya mahala pa kazi kwa kipindi cha wiki mbili, ambayo yamegharamiwa na serikali.

Amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuendeleza kuhamasisha usalama kazini kwani kauli mbiu ya mwaka huu inasema ni ‘Tarajia jiandae kukabiliana na majanga wakati wa kuwekeza mahala pa kazi  ni sasa’.

 Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa OSHA, Khadija Mwenda amesema adha kubwa wanayokutana nayo katika usimamizi wa sheria ni uelewa mdogo wa kukabiliana na athari kazini na kupelekea matatizo ni vema wananchi kutambua mtaji wao ni usalama na afya mahala pa kazi.

“Bado kuna changamoto katika mfumo  wa kuwalinda wafanyakazi mpaka sasa ni asilimia 40 tu ndiyo wako salama mahala pa kazi,” amesema Mwenda.

Kwa upande wake Wakili Mwandamizi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ambaye alimwakilisha  Mkurugenzi Mtendaji, Mercy Sevya amesema waajiri  wanapaswa kuwaelimisha wafanyakazi wao kuhusiana na namna ya kuishi salama na kutoa mfumo salama kwa ajili ya wafanyakazi mahala pa kazi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,796FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles