29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Kassim Mganga, Enock Bella kufunga mwaka Musoma

Na Shomari Binda,Musoma

Wasanii, Kassim Mganga na Enock Bella wanatarajia kuupamba mji wa Musoma katika Tamsha la usiku wa kufunga mwaka 2020 na kuukaribisha mwaka 2021 litakalofanyika kwenye ukumbi wa Le Grand Beach.

Enock Bella

Mratibu wa Tamsha hilo, Shomari Binda maesema kuwa maandalizi yote ya tamasha hilo yamekamilika ikiwamo kuwasili kwa wasanii hao.

“Maandalizi yote yamekamilika, hivyo wanamsoma wajiandae kupata burudani kutoka kwa wasanii wetu pendwa ambao ni Kassim Mganga na Enock Bela ambao wamejiandaa vilivyo kuhakikisha kuwa wanamusima wanafunga mwaka kwa namna yake Dersemba 31,” amesema Binda.

Akizungumza kuelekea tamasha hilo, Kassim Mganga amesema amejiandaa kutoa burudani ya kutosha kwa mashabiki wake wa mji wa Musoma na vitongoji vyake.

Amesema ni muda mrefu hajafika Musoma hivyo ni muhimu kutoa burudani ya kutosha na kuushukuru uongozi wa Le Grand Beach kwa kuandaa tamasha hilo la mkesha wa mwaka mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles