25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

KASPERCZAK AWASHUKURU TUNISIA

LIBREVILLE, Camroon


KOCHA wa timu ya Taifa ya Tunisia, Henryk Kasperczak, amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa sapoti yao katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon.

Timu hiyo imeyaaga mashindano hayo baada ya kuchezea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso, kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali.

Kocha huyo alisema mashabiki walionesha ushirikiano wao kwa kiasi kikubwa lakini timu haikuwa na bahati ya kusonga mbele hatua ya nusu fainali dhidi ya wapinzani wao.

“Kutolewa katika michuano hii mikubwa inauma sana, lakini mwisho wa siku mshindi ni mmoja hatuwezi kuwa wote washindi, hivyo ni lazima tukubali matokeo.

“Sisi tulitaka kuwapa furaha mashabiki kwa kazi walioifanya tangu siku ya kwanza, lakini tumeshindwa kufanya hivyo inaumiza sana, furaha yetu kwa mashabiki ilitakiwa tushinde, lakini tumeshindwa, ni pigo kubwa kwa taifa,” alisema Kasperczak.

Tunisia walikuwa na kikosi ambacho kina wachezaji wenye uwezo mkubwa na walionesha ushindani wa hali ya juu katika hatua ya makundi hadi wakafanikiwa kufikia robo fainali, ila wameshindwa kusonga mbele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles