29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

KASHWASA njia panda, Aweso aipa wiki moja

Na Clara Matimo, Mwanza

Menejimenti ya Uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) uko katika hatari ya kupoteza kazi zao baada ya kuonekana umeshindwa kuendesha kwa ufasaha mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria na kujikuta wanashindwa kulipa madeni mbalimbali jambo ambalo limemkasirisha Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na kuamua kuwapa wiki moja wafanye tathmini ya kina ambayo itasaidia kufanya mradi huo ujiendeshe kwa faida.

Waziri Aweso ametoa agizo hilo Januari 8, 2024 alipotembelea na kukagua maendeleo ya uendeshaji wa mradi huo unasimamiwa na KASHWASA uliojengwa Kijiji cha Ihelele Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza .

Mradi huo uliozinduliwa Mei 30, 2009 ulijengwa na Serikali kwa gharama ya Sh bilioni 900  unahudumia zaidi ya watu milioni 1.9 na mifugo 146,923 kutoka zaidi ya mikoa minne ikiwemo Mwanza, Shinyanga na Tabora.

Kauli ya Aweso imekuja baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA, Mhandisi Patrick Nzamba kuomba Wizara ya Maji iwasaidie fedha Sh bilioni 2,850,000,000 kwa ajili ya kununua madawa kilo 388,800 ya kuzalishia maji na kwamba Mamlaka hiyo inadaiwa Sh bilioni 5, 442, 000, 000 jambo ambalo Waziri Aweso hakukubaliana nalo na  kuagiza kama wameshindwa kuendesha mradi huo kwa faida wamuandikie barua ili ajue namna ya kufanya kuunusuru.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (mwenye koti) akikagua mradi huo.

“Huu mradi umegharimu  Sh bilioni 900,  KASHWASA huu ndiyo moyo wa Wizara ya Maji,  Menejimenti msinijaribu mimi nyie ni watu wazima, hii ni aibu, hii ni fedheha kabisa, hivi mnazijua Sh bilioni 900, Serikali imewekeza halafu mnaomba msaidiwe kulipa madeni acheni mashala kwenye utendaji kazi siwezi kulipa madeni.

“Msipokubali kubadilika nitawatoa  hebu ashumu huu mradi ungekuwa ni mradi wako wa biashara  umewekeza Sh bilioni 900 kweli  ungeshindwa kuuendesha, Mimi Jumaa Aweso ambaye nimepewa dhamana na Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuwahudumia wananchi ili wapate maji sitakuwa kikwazo kweli  wizara iwalipie umeme, iwanunulie madawa haiwezekani, kesho nipate taarifa mtanunua vipi hivyo vitu, ukiona huwezi niandikie barua nitajua la kufanya,” alisema kwa msisitizo na kuongez.a

Mwenyekiti wa Bodi ya KASHWASA, Mhandisi Joshua Mgeyekwa kaa na bodi yako na menejimenti muwafikishie wafanyakazi wote wa Mamlaka haya niliyoyasema, jukumu kuu la kuanzishwa KASHWASA ni kuendesha mradi huu na kuuza maji ya jumla kwa mamlaka zingine zinazohusika na usambazaji wa maji kwa wananchi katika maeneo ya mijini na vijijini yasiyo na vyanzo vya maji mbadala vya uhakika,” alieleza Waziri Aweso.

Aidha, Waziri Aweso alitoa wiki moja kwa Mamlaka zote za Maji nchini kufanya tathmini na kumuandikia wanadaiwa Sh ngapi na wanadai kiasi gani  ili kuona namna ya kuendelea  kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

Awali, akizungumzia uendeshaji wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA, Mhandisi Nzamba  alisema wanahitaji dawa ya kuzalisha maji, vipuli na mitambo, fedha kwa ajili ya umeme na mishahara kwa watumishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles