25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KASHFA ZAZIDI KUMWANDAMA ZUMA

PRETORIA, AFRIKA KUSINI


CHAMA cha upinzani cha Congress of the People (Cope) kinapanga kumshitaki Rais Jacob Zuma kwa kumpatia ulinzi maalumu kwa viongozi wa ngazi za juu (VIP) aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma.

Dk. Dlamini-Zuma alipewa ulinzi wa VIP kufuatia madai ya kutishiwa maisha, ambayo polisi walikuwa wakiyachunguza.

Mwingine atakayehusishwa katika kesi hiyo ni Waziri mpya wa Polisi, Fikile Mbalula.

Cope ilieleza hatua hiyo ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi na ni haramu na kinyume cha Katiba.

“Dk. Dlamini-Zuma si mgombea urais wala mbunge anayestahili kupewa ulinzi wa VIP ambao ni maalumu kwa maofisa waandamizi wa serikali na wakuu wa mataifa wa kigeni na wake zao,” kiongozi wa Cope Mosiuoa Lekota, alisema katika taarifa.

Alisema analaani vikali vitendo vya ukiukaji sheria na Katiba vinavyofanywa na Rais Zuma na Mbalula.

“Zuma na Mbalula wanapaswa kufikishwa mahakamani kueleza sababu ya matumizi haya mabaya ya fedha za walipa kodi ‚” alisema Lekota.

Kauli ya Lekota imekuja baada ya Jeshi la Polisi kufichua Zuma aliyetangaza nia ya kuwania urais wa Chama tawala cha Africa National Congress (ANC) na ambaye ni mke wa zamani wa Rais Zuma aliendelea kupokea ulinzi wa VIP kutokana na uchunguzi unaoendelea kuhusu vitisho vilivyoelekezwa kwake.

Msemaji wa Jeshi la Taifa la Polisi Sally de Beer alikiri kuwapo kwa ulinzi wa ziada.

Lakini Meja Jenerali De Beer alikataa kueleza kiundani kuhusu aina ya ulinzi aliopewa Dk. Dlamini-Zuma na aina ya vitisho alivyopokea.

Dk. Dlamini-Zuma anaonekana kuwa na nia ya kumrithi mumewe huyo wa zamani na ameshaanza kampeni.

Aidha amekuwa mstali wa mbele kumtetea Rais Zuma dhidi ya wakosoaji wanaomtaka ajiuzulu kutokana na mlolongo wa kashfa za ufisadi, upendeleo na ubadhilifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles