23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kariakoo mkoa maalumu wa kodi

Richard Kayombo
Richard Kayombo

NA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imelipa hadhi ya mkoa maalumu wa kodi eneo la Kariakoo  Dar es Salaam kwa vile ni    kitovu cha biashara nchini.

Ikizungumzia  mapato ya Agosti 2016, TRA imesema imevuka lengo kwa kukusanya   Sh trilioni 1.158 ambako lengo lilikuwa ni trilioni 1.152 ambayo ni   asilimia 100.57.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo,  alisema jana kuwa hiyo imetokana na mikakati endelevu  ambayo mamlaka imejiwekea kuhakikisha inakusanya mapato stahiki na kwa wakati.

Alisema makusanyo hayo yametokana na matunda mazuri ya mikakati iliyowekwa  na kwamba makusanyo hayo yamevuka lengo ikilinganishwa na yale ya   Agosti 2015 ambako zilikusanywa  Sh bilioni 923.

Alisema lengo kuu wa mamlaka ni kuongeza wigo wa vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na kukusanya mapato kwa ukamilifu  kuweza kufikia lengo la mwaka wa fedha wa 2016/17 na kuvuka.

“Sambamba na hayo pia tunaomba wananchi na wafanyabiashara kuendelea kujitokeza kuhakiki taarifa zao za usajili wa namba za utambulisho kabla ya Oktoba 15 mwaka huu katika vituo husika.

Baada ya muda huo kuisha hautaongezwa muda na badala yake hatua hiyo itahamishiwa katika mikoa mingine,” alisema Kayombo.

Kayombo aliwataka wafanyabiashara wa vituo vya mafuta wawe wamefunga mashine za EFDs ifikapo Septemba 30, mwaka huu  na kwamba Oktoba mosi itaanza hatua ya ukaguzi kwa vituo vitakavyokuwa vimekaidi ili hatua zichukuliwe  dhidi yao.

Alisema katika kuhakikisha VAT inakusanywa kwa wakati, walipa kodi wote waliosajiliwa na VAT wanatakiwa kuwasilisha mrejesho wa  hesabu ya biashara zao ya kila mwezi ifikapo tarehe 20 ya kila mwezi badala ya 27 iliyokuwa ikitumika mwaka wa fedha uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles