27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

KARDINALI PENGO AREJEA NCHINI

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo (katikati), akiwasili Dar es Salaam jana akitokea nchini Marekani alipoenda kutibiwa.

 

 

Na AGATHA CHARLES – Dar es Salaam

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amerejea nchini jana akitokea New York nchini Marekani alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kurejea kwa Kardinali Pengo zilitolewa jana na Askofu Msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa kupitia akaunti yake ya mtandao wa facebook na kuweka kichwa cha habari ‘Karibu nyumbani baba Kardinali’.

Askofu Nzigilwa alisema Kardinali Pengo aliwasili jana mchana akitokea nchini Marekani na kupitia Dubai ambako alipumzika kwa siku moja kufuatia ushauri aliopewa na madaktari wake.

“Baba Kardinali amerejea nyumbani akiwa mchangamfu na mwenye nguvu za kutosha. Baba Mwadhama anawashukuru waamini na watu wote wenye mapenzi mema, waliokuwa wakimuombea na kumtakia matashi mema wakati wote alipokuwa kwenye matibabu,” alisema Askofu Nzigilwa.

Kardinali Pengo amekuwa nchini Marekani kwa matibabu tangu Mei 2, mwaka huu.

Juzi, alionekana katika picha na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, walipokutana Dubai, ambako kiongozi huyo alikuwa safarini akielekea nchini Canada.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,660FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles