24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Kardashian: North ‘kaposti’ uchafu

Kim-KardashianNEW YORK, MAREKANI

MWANAMITINDO wa Kimarekani, Kim Kardashian, amemtupia lawama mtoto wake, North West, mwenye umri wa miaka miwili, kwa kitendo cha kuweka picha ya mrembo huyo ikiwa haionyeshi maadili kwa jamii kwenye mtandao wa Instagram.

Mtoto huyo alikuwa hajui alitendalo ambapo alijikuta akiweka picha ya mama yake wakati akiwa na umri wa miaka 10.

Hata hivyo, baada ya mama yake kugundua aliamua kuitoa haraka iwezekanavyo baada ya kuanza kupokea ujumbe kutoka kwa watu mbalimbali.

“Nimeshitushwa na kitendo alichokifanya mwanangu cha kuweka picha yangu isiyofaa mtandaoni, lakini baada ya kugundua niliitoa mapema na wala siwezi kumlaumu kwa kuwa hakujua alifanyalo,” alisema Kim Kardashian.

Hata hivyo, baba wa mtoto huyo, Kanye West, amemtaka mke wake aweke simu na Ipad mbali na mtoto huyo kwa kuwa sasa anaonekana kuwa na akili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles