Kanye West kuwania urais 2020

0
546

Kanye WestNEW YORK, MAREKANI

RAPA Kanye West, amesisitiza kutaka kuwania nafasi ya urasi nchini Marekani ifikapo mwaka 2020 na anaamini anaweza kuwa Rais kama sera zake zitasikilizwa.

Msanii huyo amedai kwamba yeye sera zake zitakuwa tofauti na wagombea wengine waliopita, kikubwa atakachokisisitiza ni umoja kwa watu wote.

Kanye amedai kuguswa na unyanyasaji unaoendelea kwa sasa huku idadi kubwa ya watu wakipoteza maisha kutokana na matukio mbalimbali.

“Kuna zaidi ya watoto 500 jijini Chicago wamepoteza maisha, Polisi saba wameuawa Julai mwaka huu, haya ni matatizo makubwa sana kwa jamii, lengo la kutaka kuwania nafasi hiyo ni kutaka umoja kwa kila mtu, ninaamini hali hiyo itanifanya niwe tofauti na wagombea wengine,” alisema Kanye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here