NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kanye West, ametangaza nia ya kuwania urais wa nchi hiyo mwaka 2020.
Msanii huyo aliweka wazi mpango wake huo wakati wa utoaji wa tuzo za VMA ‘MTV Video Muzic’ nchini humo huku akiamini kuwa kutangaza huko ni maamuzi magumu kwake.
Alipojinadi alidai ana uhakika ataingia Ikulu ya Marekani yeye na mkewe mwanamitindo, Kim Kardashian.
“Natangaza rasmi kuwa mwaka 2020 nitajitupa katika kinyang’any’iro cha kuwania urais kwa imani kubwa kwamba mimi na mke wangu, Kim Kardashian tutaingia ikulu.
“Nitatakiwa kuachana na kazi zangu za muziki kwa wakati huo ili nifanikishe zoezi hilo, najua nitakutana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuzomewa lakini nimejipanga kwa kupata mafanikio.
“Hizo ni ndoto zangu na zitakuwa kweli ifikapo 2020, ndiyo maana kwa sasa nimeanza maandalizi madogo madogo,” alieleza Kanye West.