27.4 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Kanye West: kila mtu ana tatizo la akili

NEW YORK, MAREKANI 

RAPA Kanye West, amesema kila binadamu ana tatizo la akili lakini muda wake haujafika wa kusumbuliwa na tatizo hilo.

Kanye ni miongoni mwa mastaa ambao wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hilo, hivyo amedai kuwa amegundua kila mmoja analo tatizo kama hila muda wake haujafika wa kugundulika.

“Nimekuwa mmoja kati ya mastaa ambao wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la akili, nadhanii hii sio kwangu tu, kila mmoja ana tatizo kama hilo, lakini muda wake ukifika kila kitu kitakuwa wazi,” alisema msanii huyo.

Wasanii wengine ambao wamewahi kukumbwa na tatizo hilo ni pamoja na Selena Gomez, Justin Bieber, Lil Wayne na wengine wengi, lakini Kanye anaamini wapo wengine ambao sio maarufu wanasumbuliwa na tatizo la akili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles