Kanye West amuibua mkongwe Paul McCartney

0
610

NEW YORK, MAREKANI

RAPA Kanye West, amemuibua mkongwe wa muziki Paul McCartney kutoka nchini Uingereza kwa ajili ya kufanya wimbo wa pamoja.

Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 77, amekuwa kimya kwa muda mrefu lakini miaka minne iliyopita kulikuwa na taarifa kwamba yupo kwenye mazungumzo na Kanye West ili kufanya wimbo pamoja na hatimaye jambo hilo limekamilika.

“Ni kweli Kanye West alitaka kufanya kazi na mimi miaka minne iliopita, lakini haikuwezekana, nadhani sasa ni wakati wake, lakini hatutakiwi kuweka wazi kama kazi iyo imekamilika au bado.

“Kwa sasa tunafanya siri hadi kila kitu kitakapokuwa tayari, ninaamini tukifanikiwa litakuwa jambo kubwa sana na itakuwa historia kwenye muziki wangu,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here