31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kanye West akwama kuwania Urais

WISCONSIN, MAREKANI 

NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kanye West, ameshindwa kufuzu kuwa mmoja kati ya wagombea wa urais katika mji wa Wisconsin kutokana na kuchelewa kuwasilisha nyaraka zake kwa wakati.

Maamuzi hayo yalifanywa na Jaji wa Mahakama ya Brown County Circuit, John Zakowski ambapo alimuondoa msanii huyo kwenye Tume ya Uchaguzi ya Wisconsin.

Msanii huyo alitakiwa kupeleka nyaraka hizo kabla ya Agosti 4 saa 11 jioni, lakini yeye alifika kwenye ofisi hizo saa 11 na sekunde 14, wakati huo tayari mfumo wa upokeaji nyaraka umesimama.

Hata hivyo Kanye West alikata rufaa, lakini Ijumaa wiki iliopita ilisikilizwa rufaa yake ila bado iligonga mwamba. Kanye West anaamini mwisho wa kuwasilisha nyataka hizo ilitakiwa kuwa saa 11:01 na sio kamili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles