Kanye West ajitoa kwenye siasa

0
1277

NEW YORK, MAREKANIRAPA Kanye West, ametangaza kuachana na mambo ya siasa na kuweka wazi kwamba alikuwa anatumika na sasa ni wakati wa kufanya mambo yake.

Wiki tatu zilizopita msanii huyo alikwenda Ikulu ya Marekani na kukutana na rais wa nchi hiyo, Donald Trump, lakini mapema wiki hii ameamua kufunguka sababu za kuachana na siasa.

“Kwa sasa macho yangu yanaangalia mambo mengine, ukweli ni kwamba nilikuwa natumika kwenye siasa na kusambaza ujumbe ambao nilikuwa siuamini, lakini sasa ni wakati wa kufanya mambo yangu kama vile ubunifu, biashara na kusaidia kutoa ajira,” alisema West.

Hata hivyo, msanii huyo aliwahi kutangaza kuwa yupo kwenye mipango ya kuja kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. West alijiongezea maadui baada ya kuonekana akiwa anasapoti vitendo cha Rais Tramp.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here