22.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Kanye West afikiria kumpa talaka mkewe

WYOMING, MAREKANI

INAONEKANA hali si shwari ndani ya  ndoa ya Kanye West na Kim Kardashian, baada ya rapa huyo kutoa shutuma nzito kwa mkewe na mama mkwe wake, Kris Jenner.

Kanye West ametumia mtandao wa Twitter, kuzungumza mambo mbalimbali likiwamo la familia ya mkewe kumfanyia vitendo vya kibaguzi na kumtenga na wanawe huku mkwewe akiwapeleka watoto wake kwenye maisha ya kishetani.

Mapema jana, Kanye West alitumia tena mtandao huo kusema amekuwa akitaka kumpa talaka mkewe mara baada ya Kim Kardashian kukutana na Meek Mill kwenye hoteli moja kujadili haki za wafungwa.

“Ni imani ya kibaguzi kwamba watu weupe wapo juu zaidi ya weusi hivyo wanatakiwa kuheshimiwa kuliko wengine. Nilitaka kumpa talaka Kim tangu alipokutana na Meek Mill kwenye hoteli ya Warldof kuzingumzia mfumo wa magereza, Meek ni mwanangu namheshimu ila Kim alitoka nje ya mstari,” alisema Kanye ambapo wengi wameanza kuhisi jamaa amerudi kwenye matatizo yake ya akili ndio maana anaongea mambo yasiyoeleweka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,647FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles