27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Kanyasu ahimiza wananchi kuchangamkia maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji Geita

Anna Ruhasha, Geita

Mbunge Geita Mjini, Constantine Kanyasu amewataka wananchi kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Geita kufika katika maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye sekta ya madini ili kupata elimu itakayowasaidia kubadilisha  mfumo wa maisha yao hasa kufanyabiashara itakayowaongezea kipato.

Muonekano ya baadhi ya mabanda yaliyopo katika maoenesho hayo.

Kanyasu ameyasema hayo Ijumaa Septemba 17, alipofika katika maonesho hayo na kutembelea mabanda mbali mbali yaliyopo katika maonesho hayo kwa malengo ya  kutoa elimu kwa wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika maonyesho hayo ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji, Kanyasu amesema kwa miaka minne mfululizo maonesho yanayofanyika  mkoani humo yameleta heshima na kuwahimiza wananchi kuyatumia kwa faida ikiwamo kujielimisha.

“Haya ni maonesho ambayo yanatupa heshima sisi wananchi wa Geita na Mji wa Geita sababu sasa yameandaliwa hapa mwaka wa Nne sasa, lakini yameshirikisha  vyombo na tasisi muhimu katika maendeleo ya nchi. Ukiangalia hapa leo mtu anayetaka kufanyabishara anapata elimu, anayetaka kupata huduma kutoka kwenye taasisi yoyote anapata na kwa wakati.

“Hivyo tuendelea kuyatumia maonyesho haya ambayo yamekuwa yakiimarika kila mwaka na kuchukua sura ya mikataifa na kuhamasisha washiriki wa nje ya nchi,” amesema Kanyasu.

Aidha, ametumia nafasi hiyo pia kuipongeza serikali ya mkoa pamoja na Wizara ya  adini  kushiriki kikamilifu kwa kuhakikisha maonesho hayo  yanakuwa kivutio  cha  kuelimisha jamii kwa masula mbali mbali ya kimaendeleo.

“Maonesho haya siyo ya kuonyeshana wao wenye mabanda bali ni kukutanisha wadau mbalimbali kutoka kwenye nyanja tofautitofauti,” amesema Kanyasu.

Wakati huohuo, Kanyasu ameupongeza mgodi wa Geita Gold Mine(GGM) kwa kuendelea kuwa wadhami wa maonesho hayo kwa kipindi chote ambapo amesema  yeye kama mbunge wa Geita Mjini anafahamu vizuri mchango wa mgodi huo kwenye jamii.

Maonesho hayo yamebeba kauli mbiu ya “Sekta ya madini kwa ukuaji wa  uchumi na  maendeleo ya watu”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles