LONDON, England
Kante alishindwa kujiunga na timu ya taifa ya Ufaransa baada ya kukutwa na maambukizi ya Corona, wakati James alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu (enka) aliyopata walipoivaa Manchester City.
HABARI njema kwa kikosi cha Chelsea ni kwamba kiungo wake, N’Golo Kante, sambamba na beki wa kulia, Reece James, wameungana na wenzao katika mazoezi ya kujiwinda na mchezo wa wikiendi hii dhidi ya Brentford.
James aliuanza vizuri msimu huu, ambapo kabla ya kuumia alishaifungia Chelsea bao moja na kutoa ‘asisti’ nne katika mechi sita pekee.
Aidha, kinachoweza kuwa kinampasua kichwa kocha wa timu hiyo, Thomas Tuchel, ni hali ya Romelu Lukaku aliyeshindwa kuungana na timu ya taifa ya Ubelgiji kutokana na majeraha ya misuli.