23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kanisa lawapa wazee chakula wabaki ndani kukabili corona

TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

JUMUIYA ya Kinondoni ya kanisa la Enlighted Christian Gethering Church (ECG) imetoa elimu ya kujikinga na virusi vya Corona kwa wazee na watu wenye majitaji maalumu.

Sambamba na hilo pia wametoa msaada wa vyakula na dawa za kutakasa mikono kwa wahitaji hao ili wabaki nyumbani kuepuka kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Mchungaji wa Jumuiya hiyo, Douglas Kimala alisema wameamua kuwaangalia wazee kwa kuwa inadaiwa kuwa ndio wanaoathirika zaidi na ugonjwa huo kutokana na kinga zao kuwa chini.

Alisema pia wazee ndio wazazi na walezi wa eneo husika hivyo wao kama jumuiya wanaamini kuwa wamepata wazazi wapya.

“Tunatambua kuwa ugonjwa huu unawaathiri zaidi watu wenye umri mkubwa hivyo tumetoa elimu kwa wazee hawa na kuwapa vitakasa mikono watakazotumia wawapo mbali na maji ya kunawa,” alisema Mchungaji Kimala.

Alisema wamewapatia msaada wa chakula ili wasihangaike kutoka katika kipindi hiki cha tishio la corona na kuwashauri watulie majumbani.

Alisema kanisa lao linaamini katika kutoa na ndio chanzo cha kubarikiwa hivyo wameamua kupata baraka zitokazo kwa wazee.

Aidha alisema kanisa hilo limeweza kuvuta umeme katika ofisi ya serikali ya mtaa wa Minazini baada ya kutembelea na kuikuta haina nishati hiyo.

Naye mmoja wa wazee hao, Mwanaidi Ally alisema wanashukuru kwa elimu hiyo, vitakasa mikono na vyakula ambavyo vitawawezesha kujikinga na ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles