30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Kangi Lugola, Kingu wahojiwa Takukuru, Masauni, Andengenye nao kuhojiwa

Ramadhani Hassan, Dodoma

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu wamehojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) jijini Dodoma.

Hatua hiyo inatokana na kashfa ya watendaji wa wizara hiyo kutia saini makubaliano ya zabuni ya kununua vifaa vya zimamoto na uokoaji vyenye thamani ya Euri 408 (sawa na Sh trilioni moja) kutoka kampuni moja nje ya nchi bila kufuata sheria.

Lugola alifika katika Ofisi ya Takukuru leo Ijumaa Januari 31, mapema saa 1.24 asubuhi ambapo aliingia kupitia geti kuu akitembea kwa miguu.

Mara baada ya kufika geti la ndani aliwasalimia baadhi ya waandishi walioweka kambi katika ofisi hizo kwa bashasha; “hamjambo, hamjambo, hamjambo wote…”

Pamoja na Lugola na Kingu, wengine wanaotarajiwa kuhojiwa na Takukuru leo ambao wanahusishwa na kashfa hiyo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni na aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles