24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Kangi Lugola asema serikali bado inawasaka waliomteka Mo

RAMADHAN HASSAN-DODOMA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Serikali inaendelea kuwatafuta watu waliomteka mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’.

Mfanyabiashara huyo alitekwa Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Colessium iliyopo Masaki jijini Dar es salaam na kupatikana Oktoba 20 mwaka huu kwenye viwanja vya Gymkhana Jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Dodoma leo Jumapili Oktoba 28, Waziri Lugola, amesema bado msako unaendelea kuwatafuta wale wote waliomteka mfanyabiashara huyo.

“Niendelee kuwasihi ndugu zangu, mmekuwa mkitaka sana kujua tunaendeleaje kuwatafuta watekaji wa Mo, mimi nimeendelea kuwaambia kwamba Jeshi la Polisi linashughulika na matukio yote ambayo yametokea na kama kuna matukio yametokea ya mtu kupotea haonekani wote hao kwa ujumla wao tutayashughulikia.

“Wale ambao hatujawapata bado Jeshi la Polisi tunaendelea kuwatafuta hadi yule wa mwisho atakapotiwa mbaroni kwa hiyo ninyi msidhani kwamba hatuwatafuti kila mkiuliza mnaulizia Mo tu tunaomba muwe waangalifu,” amesema.

Kugola pia amesema hatua hiyo italeta dhana kwamba watu wa kawaida wanapopata matatizo hawana thamani au pengine serikali haiwatafuti wale waliofanya uhalifu, na kuongeza kuwa kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi hawezi kuacha hilo likaendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles