25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Kamwelwe aiagiza TCAA kuimarisha usafiri wa unga

LEONARD MAG’OHA – DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaac Kamwelwe, ameiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kukutana na madereva teksi, wahudumu wa hoteli na waongoza utalii ili kuongeza ufanisi wa sekta ya usafiri wa anga nchini.

Akizungumza katika kongamano la pili la wadau wa sekta ya usafiri wa anga Dar es Salaam juzi, Kamwelwe alisema watoa huduma hao ni watu muhimu katika shughuli za utalii na usafiri wa anga, kwa sababu wana mawasiliano ya watalii wengi ambao wamewahi kutembelea nchini.

 “Hamza (Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari) nendeni Arusha, Kilimanjaro na Mbeya mkutane na ‘taxi drivers’, ‘tour guiders’ na wahudumu wa hoteli, mtapata mambo ya ajabu, mnaweza kukuta kijana ana namba 200 za watalii.

“Watalii ni watu wasiopenda kutumia muda mwingi safarini na sisi hivi karibuni tunakuwa na ndege za moja kwa moja,” alisema Kamwelwe.

Alisema wizara yake iko kwenye hatua za mwisho za mazungumzo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ili ianze kutoa mikopo kwa wanafunzi wa fani za urubani na uhandisi wa ndege kuwezesha kuandaa wataalamu wa ndani.

Aidha alilitaka Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuongeza safari moja ya ndege kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam itakayokuwa ikitoa huduma mchana tofauti na sasa ambapo kuna safari tatu wakati wa asubuhi na jioni.

Aliongeza kuwa huenda kuanzia Julai shirika hilo likaanzisha safari ya kutoka Mwanza kwenda barani Ulaya na kufungua fursa kwa wafanyabiashara kutumia soko la samaki lililopo nchini humo.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari, alisema kongamano hilo litawawezesha wadau kuendelea kujitafsiri na kuielewa sekta ya usafirishaji wa anga na kujua kama inaendana na dira ya taifa ya maendeleo ya viwanda.

“Litatuwezesha kuangalia nafasi ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji katika kuziba pengo la wataalamu katika sekta hii, kuangalia mchango na umuhimu wa mashirika madogo ya ndege katika dira ya taifa na kuangalia namna ya kukabili athari za mazingira zinazotokana na moshi wa ndege,” alisema Johari.

Aliongeza kuwa kutokana na wadau kuanza kuchangia katika mfuko wa mafunzo, kumesaidia kukusanya fedha ambazo zitatumika kusomeaha marubani na wahandisi wa ndege 10 kuanzia Septemba ili kuwawezesha kuingia katika soko la ndani ambalo linakua kwa kasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,211FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles