33.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Kamusi ya kwanza ya lugha za alama kuzinduliwa nchini

NA ALLAN VICENT

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, inatarajia kuzindua kamusi ya kishwahili yenye maandishi ya lugha ya alama ili kuwasaidia wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo wasioona kusoma kwa urahisi zaidi.

Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk  Ave-maria Semakafu, alipokuwa akizindua awamu ya pili ya kuchambua alama na kupiga picha za mwisho ili kuandaa kamusi hiyo ya kwanza ya lugha za alama hapa nchini.

Alisema kamusi hiyo inatarajiwa kukamilika Agosti mwaka huu ambapo inatarajiwa kuanza kutumika katika shule zenye wanafunzi wasioona na wasiosikia.

Alisema usanifishaji wa lugha ya alama Tanzania utasaidia sana kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wasiosikia katika shule za msingi na sekondari.

Dk Semakafu alibainisha kuwa kitabu hicho kitasaidia kumalizia changamoto za kimawasiliano zilizopo kwa sasa ambazo zimekuwa zikisababisha wanafunzi kukosa nafasi ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu na hata kukosa ajira hivyo kushindwa kujikwamua kimaisha.

“Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imekamilisha zoezi la ukusanyaji misamiati ya maneno mbalimbali kutoka kwa wadau na kwa sasa hatua inayoendelea ni uchambuzi wa misamiati ili kuunda kamusi hiyo”, alisema.

Alisema Serikali inatambua umuhimu wa lugha ya alama na imeweka sera mbalimbali ili kuhakikisha lugha hiyo inatumika katika ngazi mbalimbali za elimu .

Aidha alieleza kuwa lugha hiyo itakuwa ndio lugha ya mawasiliano kama ilivyo kwa lugha za Kiswahili na Kingereza.

Awali Mkurungezi wa TET, Anet Komba alimweleza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwa Tanzania kuwa kamusi hiyo itarahisisha sana ufundishaji wanafunzi wasioona na wasiosikia pia.

Alishukuru uongozi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Askofu Mkuu Mihayo (AMUCTA) kwa kutoa eneo maalumu kwa wataalamu wanaoshiriki kuandaa kamusi hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa muda uliopangwa.

Aidha alieleza kuwa kamusi hiyo itakuwa katika vishikwambi ambavyo vitatumika kuweka nakala ya laini ya alama hizo ambapo mwanafunzi akifungua anakuta maana ya alama hiyo kwa kiswahili na kiingereza.

 Komba alibainisha kuwa malengo ya kitaifa ya elimu jumuishi ya mwaka 2000-2007 ilikuwa kuhakikisha lugha ya alama inafundishwa katika ngazi zote za elimu hapa nchini ili kumwezesha mwanafunzi kiziwi kupata elimu katika ngazi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles