24.1 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

KAMPUNI ZA SIMU ZATAKIWA KUBORESHA HUDUMA WATEJA WASIHAME

Na MANENO SELANYIKA

-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amezitaka kampuni za mawasiliano nchini kuboresha huduma zao ili watumiaji wasihame kwenda mtandao mingine.

Profesa Mbarawa amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam, wakati akizindua huduma mpya ya kuhama mtandao wa simu bila kubadili namba (MNP).

Amesema lengo la kuanzishwa kwa huduma hiyo ni kuongeza ushindani  na kuboresha huduma katika sekta ya mawasiliano ambapo mtumiaji atahama kwenda mtandao mwingine kwa hiari yake.

“Kila kampuni imeshirikishwa katika mchakato wa kutoa maoni yake hivyo msiweke mizengwe na vikwazo ili kukwamisha mtumiaji ashindwe kuhamia mtandao autakao.

Akizungumzia huduma hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Injinia James Kilaba, endapo mtumiaji atahama atakapohitaji kurudi katika mtandao wake wa awali itachukua muda wa siku 30 ili kukamilisha huduma hiyo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,644FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles