26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Kampuni za simu zaliza walalahoi ununuzi vifurushi

MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

WAKATI kampuni za simu zikiendelea na ushindani wa mauzo ya vifurushi vya bando za data na kuliza walalahoi, Kampuni ya Vodacom inaonekana kuwa ghali zaidi ikiwa mbele kwa zaidi ya mara mbili ikilinganishwa na kampuni nyingine.

Kwa mujibu wa ripoti ya robo mwaka ya sekta ya mawasiliano ya simu kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) inayojumuisha miezi mitatu ya Januari, Februari na Machi mwaka huu, Vodacom ndiyo inayoongoza kwa mauzo ya juu ya vifurushi vya data.

Katika ripoti hiyo iliyotolewa hivi karibuni, Vodacom hutoza Sh 98 kwa MB moja ikiwa imejumuisha kodi ya VAT, ikifuatiwa Kampuni ya Zantel ambayo hutoza Sh 41 kwa kila MB ikiwa ni pamoja na VAT.

Ripoti hiyo ambayo inatokana na data zilizowasilishwa na kila kampuni kwa TCRA, inaonyesha kuwa Kampuni ya Tigo na Airtel zinashika nafasi ya tatu katika tozo hizo kwa kuwa zinatoza Sh 40 kwa kila MB ikijumuishwa VAT.

Katika mtiririko huo, Kampuni ya Halotel inashika nafasi ya nne kwa kutoza Sh 26 kwa kila MB ikijumuisha VAT.

TTCL inatajwa na TCRA kuwa kampuni inayoshika nafasi ya tano katika mtiririko huo kwa kutoza Sh 14 kwa kila MB ikiwa ni nafasi ya pili kutoka mwisho miongoni mwa kampuni saba za simu zilizoorodheshwa katika ripoti hiyo

Ripoti hiyo ya TCRA inaainisha kwamba kampuni inayotoza kiwango cha chini kabisa kwa malipo ya data ni Smile ambayo hutoza Sh 6 kwa MB moja.

WATEJA WA HUDUMA ZA KIFEDHA

Katika suala la utoaji wa huduma za kifedha zinazojumuisha miamala ya kuweka na kutoa fedha kupitia mitandao ya simu, kwa Januari kampuni zote zilizotajwa zilitoa huduma kwa wateja 26,503,777, Februari zilitoa huduma kwa wateja 26,671,082 ikiwa ni ongezeko la wateja 167,305 ikilinganishwa na Januari na Machi zilitoa huduma kwa wateja 26,383,998 ikiwa ni pungufu kwa wateja287,084 ikilinganishwa na Februari.

Katika utoaji wa huduma hizo, Vodacom kupitia huduma ya M-Pesa ndiyo inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi ambapo kwa Januari ilihudumia wateja 10,326,928 na Februari wateja 10,157,671 hivyo kupungua wateja 169,257 na Machi ilihudumia miamala 10,102,681 ikiwa ni pungufu ya wateja 54,990 hivyo kupoteza wateja 224,247.

Kampuni iliyofuata kwa kuhudumia wateja wengi ni Tigo kupitia huduma ya Tigo Pesa ambapo Januari ilihudumia wateja 7,959,370 na Februari wateja 7,954,048 ikiwa ni pungufu ya wateja 5,322 ikilinganishwa na Januari, na Machi ilihudumia wateja 8,330,330 ikiwa ni ongezeko la wateja 376,282 na kuifanya kuwa na ongezeko la wateja 370,960 kwa kipindi hicho cha miezi mitatu.

Hivyo, wakati Vodacom ikipoteza wateja 224,247 katika huduma zake za kifedha, Tigo iliongeza wateja 370,960 katika kipindi hicho cha miezi mitatu.

Airtel kupitia huduma ya Airtel Money kwa Januari ilihudumia wateja 5,345,519 na Februari wateja 5,549,511 hivyo kuwa na ongezeko la wateja 203,992 na Machi ilihudumia wateja 5,626,586 hivyo kuwa na ongezeko la wateja 77,075.

Kampuni ya Halotel kupitia Halopesa Januari ilihudumia wateja 1,719,627 na Februari ilihudumia wateja 1,816,078 ikiwa ni ongezeko la wateja 96,451 na Machi ilihudumia wateja 1,853,290 ikiwa ni ongezeko la wateja 37,212 ikilinganishwa na Februari.

TTCL kupitia huduma ya T-Pesa kwa Januari ilihudumia wateja 756,352 na Februari wateja 791,805 sawa na ongezeko la wateja 35,453 ikilinganishwa na Januari, na kwa Machi ilihudumia wateja 82,588 ikiwa imepoteza wateja 709,217 ikilinganishwa na Februari.

Zantel kupitia huduma ya Ezy Pesa Januari ilihudumia wateja 395,981 na Februari wateja 401,969 ikiwa ni ongezeko la wateja 5,988 ikilinganishwa na Januari, na Machi ilihudumia wateja 388,523 ikiwa ni pungufu ya wateja 13,446 ikilinganishwa na Februari.

Kampuni ya Smile haikuhudumia mteja yeyote katika huduma za kifedha katika kipindi hicho cha miezi mitatu.

MIAMALA NA VIWANGO VYA FEDHA VILIVYOHAMISHWA

Katika kupindi chote cha miezi mitatu, wateja wa kampuni zote za simu walifanya miamala 270,509,343 Januari na Februari 239,345,967 ikiwa ni pungufu kwa miamala 31,163,376 ikilinganishwa na Januari na Machi 256,150,335 ikiwa ni ongezeko la miamala 16,804,368 ikilinganishwa na Februari.

Kwa viwango vya jumla vya thamani ya kifedha kwa miezi hiyo, Januari ilifikia Sh 9,335,656,546,643 na Februari Sh 8,306,321,832,279 ikiwa ni pungufu ya Sh 1,029,334,714,364 ikilinganishwa na Januari, na Machi Sh 9,017,884,846,866 ikiwa ni ongezeko la Sh 711,563,014,587 ikilinganishwa na Februari.

Vodacom ndiyo iliyoongoza kwa viwango vikubwa vya uhamishaji fedha kupitia M-Pesa ambapo Januari ilihamisha miamala 124,414,825 na Februari 101,360,184 ikiwa ni pungufu ya miamala 23,054,641 ikilinganishwa na Januari, na  na Machi ilifanya miamala 106,352,098 ikiwa ni ongezeko la miamala 4,991,914 ikilinganishwa na Februari.

Miamala hiyo ya M-Pesa kwa Januari ilifikia kiwango cha Sh 5,450,561,266,308 na Februari Sh 4,675,239,545,169 ambayo inaainisha upungufu wa Sh 775,321,721,139  na Machi Sh 5,084,530,555,683 ikimaanisha ongezeko la Sh 409,291,010,514.

Tigo ilifuatia kwa viwango ambapo kupitia Tigo Pesa Januari ilifanyika miamala 78,991,516   na Februari miamala 70,074,203 ikiwa ni upungufu wa miamala 8,917,313 na Machi miamala 75,107,094 ikiwa ni ongezeko la miamala 5,032,891.

Miamala hiyo ya Tigo Pesa kwa Januari ilikuwa na thamani ya Sh 2,051,344,393,852  na Februari Sh 1,846,759,373,602 ikiwa ni upungufu wa Sh 204,585,020,250  na Machi Sh 1,995,840,604,555 ikiwa ni ongezeko la Sh 149,081,230,953.

Airtel ilishika nafasi ya tatu kupitia huduma yake ya Airtel Money ambapo Januari miamala iliyofanyika ilifikia 49,979,065 na Februari 50,643,194  ambayo ni ongezeko la miamala 664,129 na Machi miamala 56,914,579 ambayo ni ongezeko la miamala 6,271,385.

Miamala ya Airtel kupitia Airtel Money kwa Januari ilikuwa na thamani ya Sh 1,568,389,507,046  na Februari Sh 1,511,952,671,962 ambayo ilikuwa ni pungufu kwa Sh 56,436,835,084 na Machi Sh 1,642,225,613,794 ambayo iliakisi ongezeko la Sh 130,272,941,832.

Ilifuatiwa na Halotel ambapo kupitia Halopesa Januari ilifanyika miamala 13,333,676  na Februari 13,585,755 ambayo ni ongezeko la miamala 252,079 na Machi miamala 14,809,315 ambayo ni ongezeko la miamala 1,223,560 ikilinganishwa na Februari.

Miamala hiyo ya Halotel kupitia Halopesa kwa Januari ilikuwa na thamani ya Sh 164,608,868,885 na Februari Sh 173,248,128,211 ambayo ni pungufu kwa Sh 147,284,056,064 ikilinganishwa na Januari na Machi Sh 194,598,762,724 ambayo ni ongezeko la Sh 21,350,634,513 ikilinganishwa na Februari.

Zantel kupitia Ezy Pesa Januari ilifanya miamala inayofikia 2,844,783 na Februari 2,843,962 ikiwa ni pungufu ya miamala 821 na Machi miamala 2,956,294 ikiwa ni ongezeko la miamala 112,332 ilikinganishwa na Februari.

Miamala hiyo ya Zantel kupitia Ezy Pesa kwa Januari ilikuwa na thamani ya Sh 90,994,751,652 na Februari Sh 88,298,671,493 ambayo ni pungufu ya Sh 2,696,080,159 ikilinganishwa na Januari, na Machi ilifikia thamani ya Sh 89,734,186,856 ambayo ni ongezeko la Sh 1,435,515,363 ikilinganishwa na Februari.

TTCL kupitia T-Pesa Januari ilifanya miamala 945,478 na Februari miamala 838,669 ambayo ni pungufu kwa miamala 106,809 ikilinganishwa na Februari, na Machi miamala 10,955 ambayo ni pungufu wa miamala 827,714 ikilinganishwa na Februari.

Miamala hiyo ya TTCL kupitia T-Pesa kwa Januari ilikuwa na thamani ya Sh 9,757,758,900 na Februari Sh 10,823,441,842 ambayo ni ongezeko la Sh 1,065,682,942 ikilinganishwa na Januari, na Machi Sh 10,955,123,254 ambayo ni ongezeko la Sh 131,681,412 ikilinganishwa na Februari.

Kwa kampuni ya simu ya Smile, katika kipindi hicho hakuna muamala wowote uliofanyika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles