33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni za simu sasa kutoa bima za maisha, majanga

ruan ,milvikNa Mwandishi Wetu

SIMU za mkononi zinaweza kubadilisha taswira ya sekta ya bima nchini kama ilivyokuwa katika mabadiliko ya kibenki yaliyotokea mwongo mmoja uliopita.

Hiyo inatokea kufuatia kuanzishwa kwa TigoBima ambayo ni bima ya bure kwa simu inayotokana na muda wa maongezi wanaoununua wateja.

Tigo Tanzania ikishirikiana na Milvik (Bima kwa Simu) ambayo inaongoza katika teknolojia ya bima inayotumia teknolojia ya simu za mkononi katika kuchochea ujumuishwaji wa kifedha, imeanzisha huduma mpya iliyoboreshwa inayojulikana kwa jina la BimaMkononi, huduma ambayo inaweza kufikiwa na wateja kupitia TigoPesa.

Milvik imeshatoa huduma kama hiyo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ambapo ilihudumia wateja zaidi ya 500,000 kupitia muda wa hewani kama ilivyo kwa TigoBima. Huduma ya BimaMkononi ina bidhaa zilizounda kwa namna ya kipekee kama vile bima ya maisha, matibabu na ajali kwa mtu binafsi kwa wateja hai ambao wanatumia Tigopesa.

Akitangaza kuzinduliwa kwa huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin, alisema itatoa nafasi ya kujumuishwa kifedha kwa idadi kubwa ya watu wasio na bima.

“Huduma hii itasaidia kuziba pengo kati ya wateja na kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya simu katika maeneo ya mjini na vijini hapa nchini, tunaamini BimaMkononi itakuwa ni kichocheo kikubwa katika kusukuma mbele ujumuishwaji wa kifedha katika sekta isiyo rasmi kwa kuwawezesha Watanzania kuzifikia huduma za bima kutoka katika simu zao,” anasema Chaplain.

Anawataka Watanzania wote ambao hawawezi kuzifikia huduma za afya wanazozimudu au bima ya kawaida ya afya kuanza kutumia huduma hii kwa sababu inatoa ulinzi dhidi ya majanga ya kifedha na matatizo ya kiafya pamoja na familia zao.

Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanapoel, anasema kwamba kuzinduliwa kwa huduma hii kupo katika mkakati wa Tigo katika kuboresha mageuzi katika maisha ya kidijitali na kuongoza kwake katika kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu kwa kuwezesha BimaMkononi kupatikana kwa kutumia TigoPesa.

“Huduma hii mpya itakuwa ni fursa kubwa kwa wateja wa Tigo kuifikia huduma ya bima kwa urahisi kwa sababu BimaMkononi inalenga kuwapatia Watanzania njia mbadala wanayoimudu katika bima ya afya na maisha,” anasema Swanepoel.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inakadiria kwamba kupenyezwa kwa bima nchini kupo katika hali mbaya kwa kuwa kupo katika kiwango cha asilimia moja tu. Kwa kuangalia mgawanyo wake, sehemu kubwa imo kwa wakazi wanaoishi mjini kuliko ilivyo kwa sehemu kubwa ya watu ambao wanaishi vijijini.

Kwa mujibu wa Reinsurer Swiss Re, kiwango cha kuenea kwa bima ndani ya Afrika (kikipimwa kulinganana na Pato ghafi la ndani) ni asilimia 3.5 tu ambacho ni chini ya kiwango cha wastani duniani ikiwa ni asilimia 6.3.

Kutokana na hali hiyo, inatarajiwa kuwa pengo lililopo linaweza kuzibwa kwa kutumia njia rahisi ambazo zipo katika mfumo wa bima na katika hali hiyo mfumo mdogo wa bima kwa simu ya mkononi ndio unaopendekezwa.
Kwa hiyo, Tanzania ina muundo wa kipekee wa changamoto na soko la bima limeitikia kwa kuwa na suluhisho la malipo ya kipekee.

Kwa kutumia nembo inayofahamika na inayofikiwa na idadi kubwa ya wateja, Tigo inatarajia kutoa bidhaa za bima ndogo kwa mamilioni ya Watanzania wasio na bima na safari ndio imeanza.

Wachambuzi wanaona mbali kwamba kukua kwa sekta hii katika nchi hii ya Afrika Mashariki ambayo ina zaidi ya watu milioni 45 na hivyo kuonesha kuingia kwa simu kwa kiwango cha asilimia 67. Hali kadhalika bima ndogo nayo inaweza kufuata mkondo huo.

Uwezekano ni mkubwa kwamba mtu anahitaji kuwa na kampuni ya simu ambayo ni kubwa na iliyo na ubunifu katika kufanikisha hili. Lakini ni zile kampuni zilizo na ubunifu mkubwa ndizo zitakazofanikiwa vizuri,” anasema mchambuzi mmoja wa kisekta.

Ili kupata bima za maisha, afya na ajali binafsi halijawahi kuwa jambo rahisi. TigoBima inawawezesha wateja wake kujisajili kwa haraka na kwa urahisi katika bima wanayoitaka, moja kwa moja kutoka katika simu zao za mkononi. Wateja watafurahia kupata bima ya kiwango kimoja kwa waombaji walio na umri kuanzia miaka 18 hadi 65.

Kujisajili hakuna haja ya kuandika katika makaratasi ni kiasi cha kutumia dakika chache tu na mtumiaji anaweza kulipia kwa Tigopesa au kwa fedha taslimu katika kituo chochote cha huduma kwa wateja wa Tigo.

TigoBima inamgharimia mteja kulingana na kiwango cha muda wa maongezi alioutumia ndani ya mwezi. Jinsi ambavyo wateja wanavyotumia Tigopesa ndivyo kadri kiwango cha bima kinavyopanda na hulipwa ndani ya saa 72 za madai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles