30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Kampuni za mawasiliano ya simu zimeleta mapinduzi sekta ya afya

Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Oxford zimetangaza miradi mikubwa ya afya nchini ambayo utekelezaji wake unawezeshwa na Kampuni za mawasiliano ya simu hivyo kufanya huduma za afya kutolewa kwa technolojia ya hali ya juu, kisasa, haraka na ubora mkubwa.

Taarifa zilizopatikana hivi karibuni kutoka MNH na Chuo cha Oxford zinasema miradi hiyo itakaogharimu Sh.13.5 Bilioni unalenga kutoa huduma kwa kutumia teknolojia ya akili bandia za mifumo ya kompyuta ‘Artificial Intelligence (AI)’.

Taarifa hizo zimesema technolojia hiyo pia itaweza kufanya kazi kwa kugunduwa chanzo ugonjwa na athari mbalimbali za magonjwa kwa kutumia mifumo ya Kompyuta kitaalamu inajulikana na ‘Digital Pathology’.

Zimesema uwekezaji wa kisasa wa matumizi ya internet kwa kutumia simu za mkononi na tecknolojia ya mawasiliano unasaidia kuhakikisha hospitali nchini zinaendelea kujenga uwezo wa kutoa huduma bora zaidi na utaleta mapinduzi katika sekta ya afya na utoaji wa huduma wake.

Taarifa hizo, zilitaja baadhi ya miradi hiyo, ni ule wa matumizi ya programu za simu kama zile za M-Health. Na kufafanua kuwa Programu hii husaidia wagonjwa kufanya tafiti za awali za kinachowasumbua kupitia simu yake ‘mtandaoni’, ambapo mgonjwa hushirikisha dalili anaziona ama kuhisi kwa wataalamu maalumu na kusaidiwa kupata orodha ya magonjwa na njia za tiba zake sahihi.

Taarifa hizo, ziliendelea kutaja miradi mingine ya hudumwa kwa njia ya simu ambayo ilitambulishwa 2019, hutumiwa zaidi na watu waishio mazingira hatarishi kiafya kupata msaada wa kutuma ujumbe mfupi (SMS) kisha kupotea SMS zenye mafunzo namna ya kuishi na magonjwa yao au kuzingatia tiba na nyingine hutuma hata SMS kukumbusha kuhusu muda wa kwenda hospitali au kumeza dawa.

Aidha taarifa hizo zilitaja baadhi ya magonjwa kama VVU na Kifua Kikuu kwamba mapinduzi teknolojia yamesaidia utoaji wa huduma ya afya huduma ambapo imekuwa rahisi na kisasa zaidi.

Zinasema M-Health pia inasaidia watoa huduma za afya kusajili wagonjwa, kuhifadhi taarifa za afya na tiba na kuwasiliana. Mfano mwingine mkubwa wa huduma za afya kwa njia ya simu ni ule wa kampuni ya Tigo Tanzania wa kusajili watoto wanaozaliwa.

Taarifa hiyo, pia ilitaja baadhi ya mafanikio ya miradi hiyo, kuwa ni mfumo mpya wa kusajili watoto wanaozaliwa kuwa umeisaidia serikali kwa kiasi kikubwa na mpaka sasa umetumika kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa zaidi ya 4.2 milioni.

Taarifa hizo, zilishauri kuwa ili Watanzania waendelee kufaidi huduma hizi za kibunifu katika sekta ya afya, lazima sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi iendelee kukua kimtaji, kimiundombinu, kitaaluma na kifaida. Hili linawezakana kama tutaweka kipaumbele katika kuwa na sera bora zaidi siku hadi siku.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,951FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles