26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni za kigeni zinavyoshindana kwenye mafuta, gesi Afrika – 2

South_Asian_Summit_on_Gas_Trading_and_Transportation

Na FARAJA MASINDE,

LEO tunaendelea kuangalia namna ambavyo kampuni za kigeni zinavyogombea mafuta na gesi barani Afrika, ambapo tunaelezwa kuwa asilimia 33 ya mafuta na gesi asilia inayozalishwa Nigeria huuzwa katika Soko la Marekani.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba, Nigeria ndiyo nchi pekee ya Afrika yenye kampuni nyingi zainazomilikiwa na wazawa ambazo zinajihusisha na utafiti pamoja na uchimbaji wa mafuta na gesi ambapo kati ya kampuni 70 zilizopo, 38 ni za wazawa ama za ndani.

Miongoni mwa kampuni hizo ni Conoil, Nigeria LNG, Equator Exploration Ltd, Express Petroleum & Gas Ltd, Dubri Oil Ltd 8 Gabaro Close Victoria Island, Amni International Petroleum Development Co. Ltd, Famfa Oil, Nigerian National Petroleum Corporation ambalo  ni la umma, Nigerian Petroleum Development Co. Ltd ambalo pia ni kampuni ya umma, Oriental Energy Resources Limited, Pan Ocean Oil Corporation Nigeria na Sahara Group.

Kampuni nyingine ni Solgas Petroleum Ltd, South Atlantic Petroleum Ltd, Sunlink Petroleum Ltd, Brawal Shipping (Oil), Intels Services Nigeria, Ladol, Snake Island Integrated Free Zone, Department of Petroleum Resources, National Petroleum Investment Management Services na Nigerian Association of Petroleum Explorationists.

Ukiacha hizo pia kuna kampuni nyingine kama Petroleum Technology Association of Nigeria, First Fossil Nigeria, United Geo Physical, Survicom, Ana Industries Ltd, Ariboil Company Ltd, Kasolute, Melvon, Oil Data, Oil Test Services, Sowsco, WOG Allied Services Nigeria Ltd, Zukus Industries Ltd, WOG Allied Services Nigeria Ltd, Zukus Industries Ltd, na Drillog Petro-Dynamics Ltd.

Takwimu zinaonyesha kuwa nchi ya Nigeri ina kampuni kutoka kila pembe ya dunia ambazo zote zinawania rasilimali za mafuta na gesi kuanzia zile zinazotoka Marekani, Ameroka ya Kusini, Ulaya mpaka Asia.

oil2

Kampuni nyingine za kigeni zinazojihusisha na mafuta na gesi nchini humo ni Shell (Uholanzi), Texaco (Marekani), ExxonMobil (Marekani), Total (Marekani), Agip (Italia), Sinopec (China), Chevron (Marekani), Oanda (Canada), Addax Petroleum (kampuni tanzu ya Sinopec kutoka China), Conoco Philips (Marekani), Hardy Oil & Gas Plc (Uingereza), Nexen Inc (China – kampuno tanzu ya CNOOC Limited), Petrobras (Brazil), Statoil (Norway), Afren Energy Resources (Uingereza), Camac Allied Energy Resources (Marekani), CGG Veritas (Ufaransa), Global Energy Group (Scotland), Mabon Limited (Marekani) na Petroleum Geo-Services (Norway).

Kampuni nyingine ni Technip (Ufaransa), Schlumberger (Marekani), Fugro Nigeria Limited (Uholanzi – kampuni tanzu ya Fugro N.V.), Ensco Drilling Company (Nigeria) Ltd (Uingereza – kampuni tanzu ya Ensco Plc), Noble Drilling (Uswisi – kampuni tanzu ya Noble Corporation), African Petroleum Oil Field Services (Uingereza – kampuni tanzu ya Aprican Petroleum Plc), MI Swaco (Marekani – kampuni tanzu ya Schlumberger), BJ Services Company (Marekani), Ciscon (Marekani), Expro (Uingereza), Petrolog (Marekani), Roxar (Norway), Weafri (Marekani), Amosco (Uingereza), B.G. Technical Ltd (Uingereza), Emex Systems (Canada), na Socotherm Group (Italia).

Itaendelea wiki ijayo. Kwa maoni ushauri 0653045474.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles