28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni za kibiashara kuwania tuzo SDGs, Shayo hakuna atakayebaki nyuma

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shirika la UN Global Compact Network Tanzania limezindua mchakato wa kutafuta mshindi wa tuzo zitakazokuwa zinatolewa kila mwaka kwa makampuni ya kibiashara yaliyoonesha kwa vitendo mchango wake kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la UN Global Compact Network Tanzania ambaye pia ni Makamu Rais wa kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Simon Shayo akizungumza katika mkutano mkuu wa shirika hilo uliolenga kuzindua tuzo hizo za kampuni za kibiashara zinazotekeleza vema Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs.

Mchakato huo umezinduliwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban kwa lengo la kuendeleza ushirikiano kati ya wadau wa sekta binafsi na serikali katika utekelezaji malengo ya maendeleo endelevu.

Naibu Katibu mkuu huyo alisema UN Global Compact chapa ya Tanzania ambayo inajumuisha wadau wa sekta binafsi ni washirika muhimu wa Serikali ambao hufanya mapitio ya hiyari ya malengo hayo ya maendeleo endelevu.

“Mathalani mwaka 2019 Tanzania ilikwenda kutoa utekelezaji wake wa malengo na mwaka 2023 Tanzania inakwenda kutoa tena hivyo lazima ishirikiane na wadau mbalimbali na moja ya wadau muhimu  ni sekta binafsi ambao wanatusaidia utekelezaji wake.

“Wadau hawa tumewaomba waangalie hii tuzo ya kibiashara inaweza vipi kusaidia utekelezaji malengo yetu ya kitaifa lakini haya malengo yamejumuisha malengo ya maendeleo endelevu, hii ni katika kubadilisha ulimwengu na katika kutekeleza hayo ndio kuna ajenda 2030,” alisema.

Alisema serikali ya Tanzania imechagua maeneo matano ambayo ni muhimu.

Maeneo hayo ni watu, dunia, ustawi wa watu, usalama na ubia ambao unalenga kuendeleza ushirikiano kati ya serikali na wadau wa sekta binafsi.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la UN Global Compact Network Tanzania, Simon Shayo alisema tuzo hizo zinalenga kutathmini malengo 17 ya maendeleo endelevu ambayo Taifa hujipima kila mwaka.

Shayo ambaye pia ni Makamu Rais wa kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) anayeshughulikia maendeleo endelevu kwa upande wa Tanzania na Ghana alisema licha ya kwamba ulimwengu utapimwaifikapo mwaka 2030 kuona nchi zimefikia wapi kwenye maendeleo hayo, kubwa linakalopimwa ni ubia.

Alisema lengo la 17 linaitaka serikali na wadau sekta binafsi na wengine kuingia kwenye ubia wa pamoja katika kuhakikisha kwamba maendeleo yanayofanyika sasa, yanasaidia  kuhakikisha kwamba hakuna makundi au nchi zinazobaki nyuma.

“Malengo ya Maendeleo yetu yatakapofika 2030 tunataka tuone uwazi, kupungua kwa umaskini na uboreshaji wa maisha ya watu duniani pote.

“Tuna maeneo ambayo serikali imeshirikiana na sekta binafsi na serikali imechagua malengo matano ambayo itajipima na kuonesha pia nini mchango wa sekta binafsi kufikia malengio haya.

“Kwa hiyo malengo mengi kama mnavyoona kwenye mpango wa taifa wa maendeleo na kwenye mpango wa 2025 serikali inafanya vizuri, licha ya kwamba yapo maeneo ambayo tulicheleweshwa na madhara ya janga la UVIKO-19 lakini kama nchi na wadau wake tuna hatua ambazo tumechukua kuhakikisha kwamba tunapiga hatua,”alisema.

Alisema maeneo hayo ambayo Taifa limepiga hatua ni elimu, maji na maeneo mengine wanaamini kufikia 2030 kama nchi inayoendelea itakuwa imepiga hatua kubwa.

Alisema kitendo cha wadau wa sekta binafsi kukutana na Serikali kufanya mapitio ya taarifa ya pamoja ni udhibitisho kwamba kuna ushirikino mzuri.

“Mfano miradi yote ya maji utekelezaji wake unaandaliwa na kuadhiliwa na serikali, sekta binafsi pia na wadau wa maendeleo.

Alisema hilo ni moja ya eneo ambalo Serikali imeonesha kupiga hatua kubwa.

“Lakini pia katika suala la usawa wa kijinsia kama nchi tumepiga hatua kubwa, ukiondoa suala la asilimia 50/50 utaona hata kwenye miradi ya maendeleo tumegusa watu wote bila kumuacha mtu pembezoni.

“Hivyo kama sekta binafsi tunayo nafasi kuendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha kwamba kila moja katika malengo haya lile la 16 na 17 la ubia tunapiga hatua,” alisema.

Alisema UN Global Compact ingependa makampuni ya kibiashara yatizame mwenendo wao ili lengo lisiwe faida pekee bali iwe  faida endelevu kwa maaa kwamba faida ya kampuni na biashara zake zionekana kugusa watu.

“Pia zionekana kulinda dunia na vizazi vijavyo, zionekane kuleta ustawi kwa watu wote, zionekane ni biashara zinazojenga ubia na serikali na mwisho tunaamini biashara na sewrikali zitaleta maendeleo,” alisema Shayo.

Aidha, mbali na tuzo hizo alisisitiza kuendeleza kuwapo kwa mijadala kuhusu taarifa ya hiyari ambayo Tanzania ni moja ya nchi 42 ambazo zitatoa taarifa kwa hiyari kuonesha wamefikia wapi kwenye utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu itakauofanyika Julai mwaka huu nchini Marekani.

Kwa upande wake Mjumbe wa Shirika hilo la UN Global Compact chapa ya Tanzania, 

Anna Henga alisema uwepo wa chapa hiyo unalenga kutatua changamoto mbalimbali zinazohusu uwekezaji na watu wanaopokea wawekezaji.

Alitolea mfano wa changamoto hizo kuwa ni masuala ya fidia kwa watu wanaofikiwa na uwekezaji, kodi kwa kampuni zinazowekezaji pamoja na malalamiko mengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles