24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni za gesi zajitosa mapambano ya corona

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni za Kimataifa za Gesi na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), zimetoa mchango wa Sh milioni 383 kwa serikali kwa ajili ya vifaa tiba na vya kujikinga na virusi vya corona.

Fedha za vifaa hivyo ambavyo vimeelekezwa kwa watumishi wa afya na watoa huduma ulipokelewa jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni hizo ambazo zimeshirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio alitoa mchanganuo wa mchango uliotolewa na kila kampuni ambapo TPDC ilitoa Sh milioni 20, Wentworth Gas Ltd milioni 100, Washirika wa Kitalu cha Mnazi-Bay milioni 200 na Maurel&Prom Tanzania Ltd milioni 100.

Wengine ni Kampuni ya, Kampuni ya Shell Tanzania na Wabia wenzake kwenye Kitalu ¼ (milioni 93) na Kampuni ya Pan African Energy (milioni 70).

“Tumetoa mchango huu ili kutimiza azma ya serikali ya kuchangia mapambano dhidi janga la corona na kuisaidia katika vita hii.

“Itakumbukwa Machi 26 mwaka huu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, kupitia barua yake aliziomba taasisi za serikali, kampuni, sekta binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo kuongeza nguvu katika kushiriki vita dhidi ya janga la corona hapa nchini, nasi tumeitikia wito huo kwa mchango huu,” alisema Mataragio.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Wentworth Gas Ltd, Kanda ya Tanzania, Richard Tainton alisema wanayo furaha kuwa sehemu ya mchango wa mapambano dhidi ya janga hilo ambalo limeua watu wengi duniani.

Akipokea msaada huo, Ummy Mwalimu alisema anashukuru kwani watumishi wa afya ndiyo wako kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles