27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Kampuni yazindua ‘Smartphone app’

simu
simu

Na Hadia Khamis, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Uuzaji na Ununuzi wa bidhaa kwa njia ya mtandao  ya Kaymu Tanzania, imezindua ‘Smartphone app’ mpya katika simu za Android kwa ajili ya kuboresha huduma zake.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaama jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kaymu Tanzania, Erfaan Mojgani, alisema programu hiyo ina matumizi yote yanayotakiwa  kuwawezesha wanunuaji kutimiza muamala wowote wanaohitaji.

Alisema katika ‘app’ hiyo mtumiaji anaweza kutembelea maduka na kuangalia   bidhaa mbalimbali, kuweka oda na hata kuwasiliana moja kwa moja na wauzaji wa bidhaa.

Mojgani alisema kampuni hiyo imezindua huduma zake za kwanza katika programu ya simu nchini, hivyo itawawezesha watumiaji wa Android kununua  bidhaa na kuweka oda moja kwa moja kupitia simu zao za viganjani.

“Wauzaji nao watapata fursa ya kusimamia maduka na oda zao kwa haraka na urahisi zaidi.

“Programu hiyo inapatikana kwenye ‘Google Play Store’ hivyo haina makato yoyote ya fedha kwa watumiaji wa ‘smartphone’ hasa wale wanaotumia mtandao wa Tigo,” alisema Mojgani.

Alitaja faida zake kuwa ni pamoja na kurahisisha uwekaji wa picha za bidhaa mpya, urahisi wa kusimamia akaunti zao, kuhariri orodha ya bidhaa na kuona mauzo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles