29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya Meridianbet Tanzania yatoa mkono wa pole.

Hii Ni Familia Yetu Sote!

Ni desturi ya kampuni ya Meridianbet kurudisha kwa jamii inayoizunguka. Katika kuendeleza utamaduni huu, Meridianbet inaungana na familia ya Bi. Zainabu Mohamed ambaye anasumbuliwa na tatizo la kansa.

Bi. Zainabu ambaye ni mkazi wa Buza, Dar es Salaam, amekuwa akisumbuliwa na kansa kwa takribani miaka 2 tatizo ambalo linamfanya ashindwe kukaa au kusimama na badala yake, amekuwa ni mtu wa kulala kwa muda wote asiyeweza kujisaidia kwa chochote.

Katika kufanikisha jitihada za matibabu na kuguswa na hali aliyonayo Bi. Zainabu, Meridianbet kwa kushirikiana na Global Tv walifika nyumbani kwa mgonjwa huyu na kumpatia mkono wa pole ikiwa ni pamoja na mahitaji muhimu anayoyahitaji kwa sasa. Pia, Meridianbet imechangia kiasi cha fedha ambacho kitaongeza nguvu kwenye gharama za matibabu ambayo anayahitaji ili awezekurejea kwenye hali yake ya kawaida na kupona tatizo linalomsumbua.

Akizungumza baada ya kupokea msaada kutoka Meridianbet, Bi Zainabu aliishukuru kampuni hiyo kwa kutumia muda na rasilimali zake ili kufanikiwa kufika nyumbani kwake na kumsaidia kwa kidogo walichonacho. Pia, Bi Zainabu aliitumia nafasi hiyo kuiomba jamii nzima ya Watanzania kuweza kujitokeza na kumsaidia kwa chochote watakachoweza ili awezekuendelea kupata matibabu ya kansa akiamini kuwa bado ananafasi ya kurejea kwenye hali yake ya awali kabla ya kupata tatizo hili.

Kwa upande wa Meridianbet wakiwakilishwa na Bw. Amani Maeda ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii, alizungumzia kuguswa kwao na hali ya Bi Zainabu ambaye walimuona kupitia kipindi cha Global Jamii na kama kampuni, waliona kuna kila sababu ya kuungana nae na kumsaidia kwenye matibabu ambayo anayahitaji.

Huu ni muendelezo wa kampuni ya Meridianbet kuungana na jamii yote hasa kwa wenye mahitaji ili kurejesha tumaini la maisha kwa waliopoteza matumaini kwa sababu mbalimbali.

Kama mwanajamii, Meridianbet na familia ya Bi Zainabu Mohamed wanakualika katika kuchangia huduma za matibabu na kujikimu katika mahitaji ya kila siku ya Bi Zainabu ambaye yupo kitandani kwa miaka 2.

Unaweza kuwasilisha mchango au kuwasiliana na familia ya Bi Zainabu kupitia namba 0652837297.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles