23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Kampeni ya kutoa chanjo ya Corona yaahirishwa DRC

DRC, Kongo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ilipokea dozi milioni 1.7 za chanjo ya AstraZeneca wiki iliyopita kama sehemu ya mpango wa shirika la Afya Duniani wa Covax.

Hata hivyo, nchi hiyo imeamua kuahirisha kuanza kwa kampeni yake ya chanjo, ambayo ilitarajiwa kuanza Jumatatu hii Machi 15.

Hii ni hatua ya “tahadhari” kama nchi kadhaa, kuanzia nchi za Kaskazini mwa Ulaya, ambazo zimeamua kusitisha kampeni ya chanjo ya AstraZeneca baada ya kuona dalili ya kuganda kwa damu kwa baadhi ya watu waliopewa chanjo hiyo.

Waziri wa Afya wa DRC, Eteni Longondo, amesema: “Tumefanya mpango kuhusiana na kampeni ya chanjo ambayo ingelianza pia Machi 15, 2021, lakini kwa bahati mbaya kabla tu ya zoezi hilo, kuna nchi ambazo zilisitisha kwa tahadhari zoezi hilo kwa sababu iligundulika kuwa baada ya kutumia chanjo hiyo kulitokea baadhi ya matatizo na pia vifo. Kufikia sasa hakuna ushahidi kuwa matatizo haya yanahusiana na chanjo ya AstraZeneca. “

Waziri wa Afya wa DRC amebaini kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo; “kama tahadhari, itasitisha na kuahirisha tarehe ya kuanza kwa kampeni ya chanjo,”.

Wazo hilo, alisema waziri huyo, ni kuzipa “timu za kisayansi hapa nchini muda za kutathmini takwimu hizo na timu kutoka nchi za Scandinavia kuweza kufikia hitimisho. Ikiwa hakuna sababu na uhusiano wowote wa chanjo hii … ninaamini kwamba tutaanza kampeni ya chanjo ” , amesema waziri Longond.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles