23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Kampeini Elimu ya SGR yaanza Simiyu

Na Derick Milton, Simiyu

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanza zoezi la utoaji kampeini maalumu kwa wananchi wanaopitiwa na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR awamu ya Kwanza kipande cha tano Mwanza – Isaka km 341 ambacho kinagharimu kiasi cha Sh trilioni 3.06.

Kipande hicho cha tano Mwanza – Isaka ujenzi wake unapita katika kata za Malampaka, Mwasusa na Bai zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, ambapo Shirika hilo limeanza kutoa elimu hiyo kwa wananchi wa kata hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo, Meneja mradi wa kipande cha Mwanza-Isaka, Mwandisi Machibya Masanja amesema kuwa baada ya elimu kutolewa kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza sasa ni zamu ya wananchi wa mkoa wa Simiyu.

Amesema kuwa katika utekelezaji wa mradi huo TRC inafanya kampeini maalum ya utoaji wa elimu juu ya mradi ambao unalenga kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya Reli nchini.

Ameongeza kuwa kampeni hiyo inasimamiwa na timu ya mawasiliano kutoka katika shirika hilo ambayo inajunuisha watalaamu kutoka vitengo vya uhandisi, Ardhi, Masula ya kijamii, mazingira pamoja na ulinzi na usalama wa Reli.

“Lengo kuu la kampeini hii ni kuwapa wananchi uelewa sahihi juu ya masuala mbalimbali yanayohusu mradi pamoja na fursa zake wakati wote wa ujenzi ikiwa pamoja na kuwaandaa wananchi na hatua zinazofuata za utekelezaji wa mradi ikiwemo tathimini na ulipaji wa fidia,” amesema Mhandisi Masanja.

Ameongeza kuwa kupitia elimu hiyo wananchi watapata uelewa juu ya ujenzi wa reli, utunzaji wa mazingira taratibu zinazotakiwa katika fidia ya maeneo yao yanayopitiwa na mradi, matumizi bora na sahihi ya fedha za fidia pamoja na faida za mradi wakati wa ujenzi na kabla ya ujenzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa huo, David Kafulila ambaye alikuwepo katika mkutano huo ametaka wananchi wa kata husika kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni hiyo ili kupata uelewa zaidi wa mradi.

Aidha, Kafulila amewahakikishia fidia kulipwa kwa mujibu wa sheria na zaidi kuwaomba wachangamkie fursa za biashara wakati wa ujenzi hususani eneo la Malampaka ambapo kambi kubwa ya ujenzi inajengwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles