30.4 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kamishna wa Uhifadhi TAWA ala kiapo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa, amemuapisha, Mabula Misungwi Nyanda kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), katika hafla iliyofanyika Machi 14, 2023, katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara Mkoani Lindi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa.

Akizungumza baada ya hafla ya uapisho na uvalishaji wa cheo kipya cha kijeshi kwa Kamishna wa Uhifadhi, Mchengerwa amempongeza Kamishna Mabula na kumtaka kuendelea kutekeleza yale mazuri yaliyofanya ateuliwa kuiongoza TAWA

“Yale mazuri uliyoyafanya ndani ya TAWA hadi kukupa sifa ya kuteuliwa uyaongeze zaidi na yawe chachu katika kuongeza usimamizi wa rasilimali ya Wanyampori na malikale,” amesema Mchengerwa.

Aidha, Mchengerwa ameagiza watumishi wote kuwa waadilifu na waongeze juhudi katika ufanyaji kazi ili kuhakikisha malengo ya Serikali kwa kupitia TAWA yanafikiwa.

Kadhalika, ametoa rai kwa wananchi wote kuheshimu sheria na kanuni za uhifadhi zilizowekwa na Serikali ili kuepusha migogoro baina ya wahifadhi na wananchi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA, Mej.Gen (Mstaafu) Hamis Semfuko.

Awali akitoa salamu za ukaribisho, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA, Mej.Gen (Mstaafu) Hamis Semfuko, alimshukuru Mchengerwa kwa kumthibitisha Kamishna Mabula ndani ya mufa mfupi tangu ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kuiongoza Wizara ya Maliasili na Utalii.

“Waziri tunakushukuru sana ulipoingia tu kwenye uongozi wako ukamthibitisha Kamishna ndani ya muda mfupi, Bodi ya Wakurugenzi inakushukuru sana kwa jambo hili,” alisema Mej. Jenerali (Mstaafu) Semfuko.

Kwa upande wake Kamishna Mabula alimuahidi Mchengerwa kutekeleza yote aliyoyaagiza sambamba na kuchapa kazi kwa bidii na kwa ubunifu ili kuhakikisha malengo ya Taasisi na Wizara yanafikiwa.

Aidha, Kamishna Mabula aliwashukuru Maafisa na Askari wote kwa ushirikiano waliompa wakati anakaimu nafasi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles