Kambi rasmi ya upinzani yaishauri wizara ya elimu

0
665

Ramadhan Hassan -Dodoma

KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imeishauri Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kuwekeza kwenye teknolojia ili kuwanusu wanafunzi ambao kwa sasa wapo nyumbani.

Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo,mwishoni mwa wiki  bungeni,Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo katika Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Susan Lyimo alisem lazima kipaumbele cha bajeti ya elimu kwa sasa kiwe ni uwekezaji kwenye teknolojia ya elimu  ili elimu iweze kuendelea kutolewa kupitia nyenzo na maarifa mengine.

“Kwa kuwa mkutano huu wa Bunge ni maalumu kwa ajili ya kuidhinisha Bajeti ya Serikali, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashauri na kupendekeza kwamba bajeti ya elimu ipangwe kwa namna tofauti na miaka mingine ili kuzingatia hali halisi ya ugonjwa wa corona ambao umeathiri sekta ya elimu kwa asilimia 100.

“Ni matumaini yetu,bajeti ya elimu itazingatia uhalisia kwamba wanafunzi hawapo shuleni na vyuoni na masomo yamesimama.

Jambo la kwanza, kambi inaishauri wizara   itenge bajeti ya kuendesha vipindi vya Kitaaluma katika redio na luninga.

Alisema ili kuwapunguzia mzigo wa gharama wanafunzi, walimu na wazazi ambao watatumia njia mbadala ya mtandao kupata elimu baada ya katazo la mikusanyiko kufuatia tishio la Corona.

Alisema  kambi hiyo,  inaitaka Serikali kuandaa mpango wa ruzuku ya matumizi ya mtandao wa internet pamoja na vipindi vya taaluma na machapisho yatakayohusika na ruzuku hiyo.

Jambo la tatu, kukuza ushirikiano wa elimu kati ya taasisi za umma na binafsi ili kutatua changamoto ya utoaji wa elimu ya masafa.

“Tungependa kujua,wizara imetumia vipi utaalamu wa taasisi zake zinazohusika na teknolojia kama vile Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na vyuo vikuu ili kuja na suluhisho la kiteknolojia la utoaji wa elimu katika kipindi hiki cha janga la corona?

“Kwa muktadha huohuo, tunaitaka Serikali itenge fedha katika bajeti hii kwa ajili ya kuanzisha na kukuza ushirikiano baina taasisi za umma na za binafsi kwa lengo mahsusi la kurahisisha upatikanaji wa elimu nchini ikiwa ni sehemu ya suluhiso la changamoto inayoikumba sekta nzima ya elimu kwa sasa (ya masomo kusimama) kufuatia janga la Corona,”alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here