27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati yapitisha makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2022/23

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2022/23 ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Bunge na Uratibu), Balozi. Dk. Pindi Chana akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Katiba na Sheria wakati wa kujadili na kupitisha taarifa Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka  wa fedha 2022/23  katika Ofisi za Bunge  Machi 23, 2022 jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Najma Giga Machi 23, 2022 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma  mara baada ya wajumbe kujadili na kuridhia bajeti katika kikao kilichohusisha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Wakurugenzi wa Idara mbalimbali, wataalamu  na taaisisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

“Tunashukuru kwa wasilisho la Bajeti hii  na wajumbe  wamesikiliza wamepata nafasi ya kutoa maoni yao katika maeneo mbalimbali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu  na shughuli za serikali kufanyika bila kikwazo na wajumbe wote wa kamati wameipitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu,” amesema Najma.

Awali katika kikao hicho Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu, Balozi, Dk. Pindi Chana aliwasilisha taarifa kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka  wa fedha 2022/23  mbele ya kamati hiyo.

Pia, Pindi alieleza mpango wa shughuli zitakazotekelezwa kwa kutumia bajeti hiyo ya mwaka wa fedha ujao 2022/23 ambapo wanakamati kwa kauli moja walipitisha randama ya bajeti na kutoa ushauri kwa wizara katika  baadhi ya maeneo yanayohitaji kufanyiwa marekebisho.

“Nitumie nafasi hii kuishukuru kamati na wajumbe kwa mawazo yao hadi kupitisha bajeti hii na nimshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu bajeti hii tunayopitisha hapa lazima ipate ridhaa ya Mkuu wetu wa Nchi,” ameshukuru Pindi.

Aidha amebainisha kwamba kupitishwa kwa bajeti hii kunatoa fursa ya utekelezwaji wa malengo, dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2020/25, utekelezaji wa Ilani na hatimaye kupitia Bunge kila mwananchi apate maendeleo na kukuza uchumi wa Taifa.

“Ni imani yangu kuwa  bajeti hii itakapopita tunakwenda kutekeleza malengo yetu, dira yetu ya maendeleo 2020/25 na hatimaye tupate maisha bora kwa kila mtanzania hivyo kwa niaba ya wizara na timu nzima ya wataalamu tunawashukuru sana kwa ushirikiano wenu,” amesema Pindi.

Akitoa elimu ya uelewa kuhusu muundo na utekelezaji wa majukumu Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Katibu Mtendaji, Dk. Godwill Wanga  alibanisha kwamba kupitia baraza hilo wapo katika mchakato wakuunganisha mifumo ya Taasisi zote zinazohudumia wafanyabiashara na kuwa  mfumo mmoja utakaosaidia wafanyabishara kufanya shuhuli zao kwa urahisi na  kutatua changamoto zinazowakabili.

“Utafiti ulifanyika namna ya kuunganisha mfumo kwa sababu iliyopo inaonyesha kuleta changamoto kwa wafanyabiashara maana kwa sasa kila taaisisi ina mfumo wake hivyo maelekezo yaliyotolewa ni kuiunganisha pamoja na taarifa zake ambapo  mtu wa NIDA au  BRELA  akitaka anaingia kwenye data base hiyo hiyo na kupata taarifa anazozitaka  ambapo hatua hii itaondoa usumbufu kwa wafanyabiashara,” ameeleza Dk. Wanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles