31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

KAMATI YA BUNGE YAISHAURI SERIKALI KUNUNUA ASILIMIA 60 YA HISA ZA AIRTEL

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mindombinu, imeishauri Serikali kununua asilimia 60 ya hisa za Kampuni ya simu ya Airtel ili kuipa uwezo Kampuni ya Simu Nchini (TTCL).

Katika taarifa ya kamati iliyosomwa na Mwenyekiti wake Prof. Norman Sigalla, inashauri kuwa Serikali iwekeze kwa kuipa fedha TTCL kwa ajili ya kupanua maiundombinu yake kwa kuwa soko la ushindani kwenye Sekta ya Mawasilaiano ni kubwa sana.

“Kwa kuwa Airtel imekuwa ikitangaza kuwa haipati faida kila mwaka, ni vyema sasa Serikali ikanunua asilimia 60 ya hisa zinazomilikiwa na Airtel ili kuweza kutumia miundombinu yake na kuongeza wigo wa maeneo yatakayofikiwa na TTCL kwa haraka,” Alisisitiza Prof. Sigalla

Aliongeza kuwa, kamati inatambua kuwa uwekezaji wa TTCL kufikia kiwango cha kuenea nchi nzima unaweza kuhitaji fedha nyingi zaidi kuliko kununua hisa asilimia 60 za Airtel.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles