26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

Kamati ya Bunge ya Utawala yatembelea miradi ya ujenzi wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria imeonesha kuridhishwa na hatua ya ujenzi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Ujenzi wa Kiwanda cha Uchapaji wa Nyaraka za Serikali Mjini Dodoma.

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene akisalimiana na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala Katiba na Sheria walipotembelea Taasisi na Idara zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria, Joseph Mhagama, Machi 18, 2023 katika ziara ambayo ililenga kujionea kile ambacho kimepangwa kwenye bajeti ya Serikali na kuangalia hatua zilizopigwa, changamoto zilizojitokeza na namna ya utatuzi wake.

“Ziara hii imetuwezesha kupata uhalisia wa hali jinsi ilivyo, ili iweze kutusaidia wakati wa kupanga bajeti, tuwe na uhalisia wa utekelezaji miradi,” alisema Mhagama.

Akizungumzia kuhusu Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Mhagama amesema upo muhimu wa Idara hiyo kuwa na mifumo rasmi ya kujisimamia bajeti yake yenyewe (kama wakala) ili isaidie idara hiyo iweze kuingia katika soko shindani.

Aliongeza kusema Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ikiweza kujisimamia katika bajeti yake, itasaidia kuongeza Makusanyo mengi ambayo yanategemewa kutoka katika Idara hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene akiwa na wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria walipotembelea kujionea Maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Tunachangamoto kubwa sana katika utengenezaji wa nembo ya Taifa: “Lazima tuwe na Mamlaka moja ya kutengeneza nembo ya Taifa na watu wengine wote waipate kupitia katika Ofisi ya Mpiga Chapa wa Serikali,” amesema Mhagama.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema anakubaliana na maelekezo ya Kamati nakwamba Wizara itatoa taarifa mbele ya Kamati hatua iliyofikia katika kuandaa mabadiliko ya sheria ili kuwezesha Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kuwa wakala.

Naye, Ahmed Ngwali Mjumbe wa Kamati, ameshauri Idara ya Mpiga Chapa Mkuu Wa serikali Kufanyia kazi mapendekezo ya Kamati mapema ili iweze kubadilishwa na kuwa wakala.

Awali, Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, George Lugome amesema Utakapokamilika mradi wa Kiwanda cha Uchapaji wa Nyaraka za Serikali itasaidia kuimarika kwa utunzaji wa kumbukumbu ikiwa ni sambamba na kuongeza ajira na kuwa sehemu ya mafunzo kwa watu wanasomea maswala ya uchapishaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,405FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles