29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya Bunge ya Bajeti yaridhishwa hatua ujenzi mradi Butimba

*Ni ule unaosimamiwa na Mwauwasa

Na Clara  Matimo, Mwanza

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imetembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Maji uliojengwa Kata ya Butimba Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kwa gharama ya Sh bilioni 82 ambapo imeridhishwa na hatua  iliyofikiwa ya asilimia 99.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo(Mwenye Kofia ngumu ya bluu) akikagua mitambo ya mradi wa maji uliojengwa Kata ya Butimba jijini Mwanza.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo unaozalisha lita milioni 48 kwa siku ambao ujenzi wake unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (Mwauwasa) hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Daniel Sillo alisema kamati yake imeridhishwa na ujenzi wa mradi huo mkubwa pamoja na hatua nzuri iliyofikia kwani umetekelezwa kwa kuzingatia viwango vya ubora.

“Ujenzi wa mradi huu umefikia hatua nzuri, hakika utakidhi mahitaji ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza pia utatatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama  kwa kiwango kikubwa kwa dhati kabisa tunampongeza sana Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suliuhu Hassan kwa dhamira yake ya dhati ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani.

“Niwahakikishie tu  wananchi wa Mkoa wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla Kamati yetu  haitokuwa kikwazo katika upatikanaji wa fedha ili miradi mingi itekelezwe na ikamilike kwa ubora na kwa wakati hasa ikizingatiwa kuwa jukumu lake la msingi ni kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo,” alisema Sillo.

Kwa upande wake Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alisema  Wizara itahakikisha miradi yote ya maji nchini inajengwa kwa ubora unaotakiwa pia inakamilika kwa wakati ili kukidhi mahitaji ya huduma ya maji kwa wananchi na kuiagiza Mwauwasa kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanaunganishwa na huduma ya maji na kusiwe na sababu zisizo za lazima katika kutimiza zoezi hilo.

“Nikuhakikishie Mheshimiwa Sillo pamoj na waheshimiwa wabunge wote wa kamati yako kwamba Wizara ninayoisimamia mimi Jumaa Aweso haitakuwa kikwazo  kwa Watanzania kutatuliwa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama  ili kufikia asilimia 95 ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa maeneo ya mijini na aslimia 85 kwa maeneo ya vijijini ifikapo mwaka 2025 kama ilivyo malengo ya Serikali.

Kamati ikiendelea kutembelea na kukagua mradi wa maji butimba jijini Mwanza.

“Tunatoa pongezi na shukrani zetu nyingi sana kwa Mheshimiwa Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha ambazo zimewesesha ujenzi wa mradi huu mkubwa wa maji ambao tayari tumeanza kushuhudia matunda yake katika baadhi ya maeneo hasa ikizingatiwa kuwa changamoto ya maji kwa Jiji la Mwanza hapo awali ilikuwa ni kubwa,” ameeleza Aweso.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles