28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya Bunge A.Mashariki yaipongeza Bandari Dar es Salaam

Na Esther Mnyika,Mtanzania Digital

Kamati ya Mawasiliano, Biashara na Uwekezaji ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, imetoa pongezi kwa Bandari ya Dar es Salaam kwa kuboresha utoaji huduma, huku ikiitaka kuongeza kasi ya kupakua na kupakia mizigo katika meli.

Wajumbe wa kamati hiyo wameyasema hayo leo Februari 8, 2024 walipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kubadilisha uzoefu katika utoaji huduma za kibandari na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohitaji ufumbuzi ili kurahisisha utoaji huduma katika bandari hiyo.

Akizungumza baada ya ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Mawasiliano, Biashara na Uwekezaji wa Bunge la Afrika Mashariki, Rutazana Francine, amesema wameridhishwa na utolewaji wa huduma lakini kuitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuendelea kuboresha.

Amefafanua kuanzia Februari 4- 7, 2024 wamekuwa katika makundi mbalimbali ya wadau ambao wanatembelea bandari mbalimbali zilizopo katika jumuiya hiyo.

“Tumezungumza masuala mbalimbali na baada ya majadiliano tumekuja katika ziara ili kuona yale tuliyokuwa tunaelezwa na wenzetu wa TPA na Bandari ya Dar es Salaam. Hata hivyo tumeshauri namna ya kuondoa changamoto ya ucheleweshwaji wa bidhaa katika bandari, tunatamani kuona changamoto hiyo inapatiwa ufumbuzi, ” amesema.

Amesema katika ziara yao wamegawanyika makundi matatu na miongoni mwa mambo wanayotaka kujua ni wanafaidikaje na utendaji kazi wa ‘centre cordial’ ambayo inahusisha nchi za Rwanda, Burundi, Congo, Uganda na Sudan Kusini.

Francine ameongeza kuwa kuna kundi lingine limeenda kukagua shughuli za utendaji kazi katika Bandari ya Mombasa.

Naye Mbunge wa Afrika Masharika kutoka Kenya, David Sankok amesema wao wameridhishwa utendaji kazi wa TPA kwa sababu wameona kuna uwezo wa kupaki kotena za mafuta kwa wingi na kuweza kusambaza nchi zote za Afrika Mashariki na eneo lingine la Bara la Afrika.

Amesema watanzania wana nafasi kubwa kuwekeza kwenye uchumi wa bluu kwa sababu wana bahari maziwa ikiwemo Tanganyika, Victoria na Nyasa ambako kunaweza kuwa na bandari kwa ajili ya bidhaa kutoka Ulaya na sehemu zingine.

“Wawekeze sana na watafute wataalamu wa uchumi wa buluu, itakuwa Tanzania yenye uchumi wa buluu na hakuna nchi nyingine Afrika yenye uchumi huu,”amesema Sankok.

Amesema wamesikia changamoto iliyopo kwa wafanyabiashara wao ni kitengo ambacho wanatengeneza sheria ili nchi ziweze kufanyakazi kwa pamoja na huduma bora.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bandari hiyo, Mussa Biboze amesema wabunge hao wamejifunza kazi kwao hivyo kuendelea kuongezeka ufanisi katika bandari hiyo na kuweka malengo.

Amesema changamoto chache ambazo wanafanyia kazi ili kurahisisha bandari ifanye kazi kwa ubora huku akifafanua kuwa mzigo ya ndani inatoka
ndani ni siku tano na nje ya nchi wana mikataba ya siku 24 na zingine siku 30

“Sisi kama Bandari tumejipanga kuweza kutoa huduma bora kwa wateja wetu wote wa East Afrika lakini pia tuwaombe kama walivyoziona changamoto ambazo wameahidi kutusaidia ikiwemo ya utungaji wa sheria zitakazosaidia ufanyaji wa biashara kuwa rahisi wazishughulikie kwa wakati ili tuendelee kutoa huduma kwa wananchi wote,”amesema Biboze.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles