29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Kama unataka kusoma Ulaya zingatia haya

Chuo Kikuu cha Freiburg, Ujerumani
Chuo Kikuu cha Freiburg, Ujerumani

Na FARAJA MASINDE,

IDADI kubwa ya wanafunzi wengi wa kitanzania na hata Afrika wamekuwa wakitamani kupata taaluma zao kwenye vyuo vikuu vya mataifa yaliyoendelea.

Hata hivyo changamoto huja kuwa ni kwa namna gani wanaweza kupata vyuo stahiki hasa vilivyoko Ulaya.

Kwasasa kila vijana watatu kati ya watano utakaokutana nao watakuambia kuwa wanataka kusoma Ulaya.

Na miongoni mwa sababu ambazo wamekuwa wakizitoa ni ile ya ubora wa elimu ambayo wanaamini kuwa inapatikana kwenye mataifa hayo yaliyopiga hatua.

Pia sababu nyingine imekuwa ikitajwa kuwa ni kuwapo kwa fursa kubwa za ajira, kubadilisha mazingira, kuimarisha mahusiano mazuri na sababu zingine.

Kama hivyo ndivyo basi haya ni mambo muhimu ya kuzingatia kama unataka kusoma vyuo mbalimbali barani Ulaya.

Ni kweli kuwa kuna mambo muhimu ya kuzingatia pindi unapokuwa unahitaji kwenda kusoma vyuo vya kimataifa nikiwa na maana ya Ulaya, hapa kuna hatua muhimu ambazo unapaswa kuzizingatia ili kuhakikisha kuwa unajipanga vyema kabla ya kwenda kusoma Ulaya.

NCHI

Ni lazima utambue kuwa unachagua nchi unayoipenda ndani ya nchi 28 za Ulaya.

Ni lazima utambue kuwa nchi nyingi za Ulaya kwasasa zinafadhili somo la kiingereza kwenye ngazi ya Shahada kwa wanafunzi wa kimataifa ambapo hii inatoa fursa kwa mwanafunzi husika kuimarisha ujuzi wake kwenye lugha hiyo.

Hii inakuwa na faida kwenye eneo lako la kazi au pindi unapokuwa unasoma, pia kwa mwanafunzi kujifunza lugha mpya kikamilifu nje ya ile anayoifahamu.

Hivyo unaweza kujifunza lugha mbalimbali kama vile kifaransa, kihispania, kijerumani kwa wakati mmoja na hivyo kufanya wasifu wako kuwa na mashiko zaidi.

MIJI, MATAWI YA CHUO

Wanafunzi wengi huwa wanapenda kusoma kwenye miji mikubwa na iliyo na pilikapilika nyingi wakiwa na maana kuwa wanaweza kujikuta nao wakifanya biashra za hapa na pale.

Hivyo ni chaguo lako kuangalia tawi gani la chuo ambalo unadhani linakuwa na faida zaidi kwako ili kuhakikisha kuwa unakuwa huru.

KOZI

Hii ni sababu muhimu kwa wanafunzi wengi pindi wanapohitaji kwenda kusoma nje kwani ni lazima uchague chuo kwa kuzingatia aina ya kozi unayotaka kusoma kwa sababu kuna nchi ambazo zimebobea kwenye baadhi ya kozi kwa maana ya taaluma.

Hivyo ni jambo la msingi kufanya uchanganuzi wa chuo kwa kuzingatia kozi unayohitaji kwenda kusoma kwani kila mji umekuwa ukibobea kwenye kozi yake kinyume na matarajio yako.

UBORA WA CHUO

Kila mtu anapenda kujiona kwenye viwango vikubwa vinavyofanywa na mashirika ya utafiti kama la THE, QS na Academic lakini ni muhimu kuzingatia umahiri wa utafiti husika.

Kwani kila shirika la tafiti limekuwa likitumia mbinu zake katika kupata vyuo bora hivyo ni jambo la msingi kuangalia chuo unachokihitaji kiko nafasi ya ngapi kwenye orodha ya ubora na kuzingatia mafanikio ya tafiti zilizofanywa na chuo husika na mafanikio ya wahitimu wa chuo husika.

Mambo mengine muhimu ya kuzingatia ni gharama na namna utakavyoweza kumudu kuangalia ufadhili japokuwa asilimia kubwa ya vyuo vikuu barani Ulaya vimekuwa vikitoa ufadhili kwa wanafunzi wa kimataifa.

Jambo jingine la msingi ni kufuatilia mafanikio ya wanafunzi waliotoka kwenye chuo unachohitaji kwenda kusoma hasa wale wa nyumbani.

Lakini pia kufuatilia urahisi wa upatikanaji wa ajira kwa wahitimu wa chuo husika ambapo kwa kiwango kikubwa haya yote utayapata kwenye tovuti ya chuo husika unachokihitaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles