24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Kala kuja na ‘Wana ndoto’

Kala Jeremiah
Kala Jeremiah

Na THERESIA GASPER,

MSANII wa hip pop, Jeremiah Masanja ‘Kala Jeremiah’ anatarajia kuachia wimbo mpya ambao utajulikana kwa jina la ‘Wana ndoto’, ukiwa umetengenezwa na matayarishaji Pablo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kala alisema wimbo huo utatoa somo, hasa kwa wale watu ambao wana ndoto za kufanya jambo fulani.

“Katika maisha ya kawaida kila mtu anakuwa na ndoto zake za hapo baadaye, lakini baadhi yao huwa wanakata tama, ila kwenye huu wimbo utawapa somo na kutimiza malengo yao,”
alisema Kala.

Kala, ambaye anatamba na wimbo wa ‘Malkia’, alisema kwa sasa hayupo tayari kuuzungumzia sana, isipokuwa amewataka mashabiki wake wakae tayari kupokea wimbo huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles