22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Kala Jeremiah: Tukumbuke maisha baada ya uchaguzi

kala-jeremiahNA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII wa muziki wa rap nchini, Kala Jeremiah, amewataka wasanii wenzake wanaoshabikia vyama mbalimbali kuelekea kwenye uchaguzi wa Oktoba 25, wakumbuke maisha baada ya uchaguzi huo.

Kala Jeremiah alisema anashangazwa na wanaojibweteka upande mmoja wa chama bila kujua maisha yao yatakuwa vipi baada ya uchaguzi kupita.

“Ni haki kwa kila mtu kuwa na mtu anayemkubali kama rais, lakini ninavyoona kuna baadhi ya watu wana ushabiki unaovuka mipaka, hofu yangu kubwa ni baada ya uchaguzi maisha yao yatakuwa vipi,” alisema Kala na kuongeza:

“Mimi kuna mtu namkubali awe rais, lakini siwezi kumkashifu wa upande nisiomkubali na hiyo ndiyo demokrasia, badala ya kuchukiana na kukashifiana kupita kiasi,’’ alisema Kala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles