Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Mapema Mwezi huu Mtanzania Abdulrazak Gurnah, ambaye ni mwandishi nguli wa riwaya, aliitangaza vyema Tanzania baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Fasihi ya Nobel kutokana na utunzi wake juu ya ukoloni mamboleo na masuala ya wakimbizi.
Ushindi huo ni wazi kuwa umedhihirisha utabiri wa Msanii wa nyimbo za kizalendo nchini Tanzania, Joash Timothy Omolo almaarufu Kaka J Wimbo wake aliorekodi mwaka 2014 unaofahamika kama Tanzania wenye maudhui ya kusifu nchi.
Akizungumza na Mtanzania Digital Kaka Jay amesema ndani ya wimbo huo aliimba kuwa ameimba ‘Tuzo ya Nobel ije Tanzania, kwa baba Nyerere nchi ya Karume, Visiwa na Bara sote ndugu moja.
Amesema wimbo wake aliorekodi mwaka 2014 uitwao Tanzania wenye maudhui ya kusifu nchi , viongozi na watu wake ulitamba katika vyombo vya habari kati ya mwaka 2014 hadi 2020.
Katika wimbo huo Kaka Jay ameimba kuwa tuzo ya Nobel ije Tanzania kwenye nchi ya hayati Julias Nyerere na Abeid Karume.
“Tuzo ya Nobel ije Tanzania kwenye ardhi ya baba yetu Nyerere na Karume visiwani na bara kwani sote ni wamoja,”aliimba msanii huyo kwenye wimbo wake alioutoa miaka saba iliyopita ukiwa umetayarishwa na Studio za Mabinda Rekcords.
Kaka Jay alimeongeza kuwa anafurahi kuona tuzo hiyo imetua kwa Mtanzania kwani ndoto yake imetimia.
“Video yangu mtu anaweza kuitazama kwa kuingia kwenye Youtube kwa kuandika jina la wimbo ambalo ni Tanzania msanii Kaka Jay.
“Lakini pia anaweza kutazama video hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram wa @kakajaytz_2007,”amesema Msanii huyo mwenye makazi yake mkoani Shinyanga.
Gus lhapa kutazama video hiyo hapa:
Mshindi wa Nobel ‘Gurnah’ ni nani
Gurnah alizaliwa na kukulia visiwani Zanzibar lakini akakimbilia Uingereza kama mkimbizi mwishoni mwa miaka ya 1960, ameandika riwaya 10 ikiwamo ya “Paradise” ambayo ilichaguliwa kuwania tuzo za Booker na Whitebread mwaka 1994.
Riwaya hiyo ina marejeo dhahiri ya riwaya maarufu ya mwandishi wa Kiingereza, Joseph Conrad ya mwaka 1902 “Moyo wa Giza” katika kuonyesha picha ya shujaa kijana asiye na hatia akiwa katika safari ya Afrika ya Kati na Bonde la Kongo.
Hadi kustaafu kwake hivi karibuni, Gurnah alikuwa Profesa wa Fasihi ya Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Kent kilichopo huko Canterbury akijikita zaidi kwa waandishi wenzake nguli kama Wole Soyinka, Ngugi wa Thiong’o na Salman Rushdie.
Joash Timothy Omolo almaarufu @kakajaytz_2007 ni Msanii wa nyimbo za kizalendo na kisiasa nchini Tanzania. Wimbo wake aliorekodi mwaka 2014 uitwao Tanzania wenye maudhui ya kusifu nchi , viongozi na watu wake ulitamba Sana katika vyombo vya habari kati ya mwaka 2014/2020.