21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

Kairuki awapiga mkwara maofisa utumishi

Angella
Angella Kairuki

 

Na Lilian Justice, Morogoro

SERIKALI imesema haitawafumbia macho maofisa utumishi wazembe watakaoshindwa kusimamia idara zao.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, alipozungumza katika kikao kilichokutanisha watumishi wa umma kutoka idara mbalimbali za Serikali.

Alisema Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wake wanapatiwa huduma stahiki pindi wanapofika katika ofisi mbalimbali na hivyo haitakubali maofisa utumishi waliopewa madaraka kuona wanashindwa kutekeleza majukumu yao  kikamilifu katika sehemu za kazi.

“Lengo kuu la kufanya kikao hicho ni kuwakutanisha watumishi wa umma kutoka idara mbalimbali ili kufanya majadiliano na kutiana ari,” alisema Kairuki.

Aliwataka watumishi hao kuhakikisha wanajiwekea utararibu wa kukusanya kero mbalimbali za watumishi walioko chini yao ili Serikali iweze kuzishughulikia kwa haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,814FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles