24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Kairuki ataka miundombinu ya uwekezaji nchini

Na MWANDISHI WETU-MBEYA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji),  Angellah Kairuki, ameiomba mikoa na halmashauri kutenga maeneo ya uwekezaji na kuyawekea miundombinu stahiki ili  kuwavutia wawekezaji nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tano katika mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya iliyomsaidia kujifunza, kujionea uwekezaji pamoja na kuzungumza na wawekezaji katika ukanda huo.

Waziri amekipongeza Kituo cha Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), kwa kuwa mfano mzuri katika  kuhamasisha  uwekezaji  na kutaka taasisi zingine kuiga mfano huo.

Alisema mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta mbalimbali  zikiwemo sekta za  utalii, kilimo na ufugaji.  

“Serikali inaweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kufanya shughuli na kukuza la pato taifa,” alisema Kairuki

Licha ya haki hiyo aliwataka wawekezaji kujisajili kwa hiari  kwenye Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) ili kunufaika na fursa zilizomo katika kituo hicho kwani wanufaika ni mwanachama pekee  waliosajiliwa  na TIC. 

“Wawekezaji tunawakaribisha TIC ili mjue fursa ziliopo nchini  na kuona namna mnavyoweza kunufaika na kituo hiki,” alisema 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa  SAGCOT, Geoffrey Kirenga, alisema kituo kitaunganisha nguvu kutoka sekta za uma na binafsi ili kutoa mchango chanya katika maendeleo ya taifa.

“Kama wadau wa sekta ya kulimo, tutashirikiana na serikali na sekta binafsi kufanikisha azma ya serikali ya awamu ya Tano  ya Dk. John Magufuli kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo ili kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda,” alisema Kirenga.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,310FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles