27.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

Kaimu Kamishna wa TAWA akagua miradi ya mamlaka hiyo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda amefanya ziara ya kikazi katika Kanda mbalimbali za TAWA ikiwemo Kanda ya Ziwa, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati na Kanda ya nyanda za juu kusini.

Ziara hiyo ya siku tano (5) ilifanyika Septemba 12 hadi 17, 2022, ililenga kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali yanayosimamiwa na TAWA.

Akiwa katika Kanda ya Ziwa, Kamishna Mabula alikagua miradi ya ujenzi wa barabara, lango la kuingilia wageni na camping site inayotekelezwa katika Pori la Akiba Kijereshi.

Vilevile katika Pori la Akiba Maswa alikagua ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 200, ukarabati wa kiwanja cha ndege Buruti, ukarabati wa kiwanja cha ndege Mbono, ujenzi wa kituo cha Askari, ujenzi wa ofisi pamoja na ujenzi wa vituo viwili vya kudumu vya kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu katika vijiji vya Malwilo (Meatu) na Lugalombogo (Itilima).

Pia katika Kanda ya Magharibi, Kamishna Mabula alikagua ujenzi wa jengo la kutoa habari (Information Center) lililopo katika Bustani ya wanyamapori Tabora (Tabora Zoo).

Vilevile katika Kanda ya Kati na Nyanda za Juu Kusini Kamishna Mabula alikagua ujenzi wa vituo vya kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu vya Mtera na Mboliboli.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, Kamishna Mabula amesema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ilipofikia na akaelekeza wakandarasi wakamilishe ujenzi wa miradi hiyo kabla ya tarehe iliyopangwa ambayo ni Septemba 31, 2022.

Miradi hiyo imejengwa kwa kupitia Fedha za Maendeleo na Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 na fedha za bajeti ya kawaida.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles