27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kagere amponza mwamuzi

Zainab Iddy

BODI ya Ligi Kupitia Kamati yake ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Tanzania (Kamati ya saa 72) imetoa onyo kwa mwamuzi Jonesia Rukyaa baada ya kubainika kuchezesha chini ya kiwango mechi ya watani na jadi Simba na Yanga uliochezwa Januari 4, mwaka huu.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Yanga  kupitia kwa nyota wao Meddie Kagere na Deo Kanda wakati kwa Yanga ni Mapinduzi Balama na Mohamed Issa ‘Mo Banka’ na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Akizungumza katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Ibrahim Mwanyela, alisema baada ya kupitia video ya mchezo mzima wa Simba na Yanga, kamati ilibaini kulikuwa na kasoro kubwa kwa waamuzi waliosababisha matokeo ambayo si sahihi.

“Matokeo hayawezi kubadilika lakini kamati imeona ili kutorudiwa kwa makosa, waamuzi Jonesia na Soud Lilla wapewe barua za onyo kali kwani hawakuweza kuzitafsiri sheria 17 za soka ipasavyo kiasi cha kutoa maamuzi ambayo si sahihi.

“Iwapo kama waamuzi hawa watakuja kufanya makosa kwa mara nyingine kamati italazimika kuwapa adhabu ya kuwafungia kuchezesha kwani kitendo cha kutotafsiri vizuri sheria za mpira kinasababisha kuinyima haki timu moja huku nyingine ikipata matokeo ambayo si haki yao,” alisema Mwanyela.

Miongoni mwa matukio yalioonekana kuleta utata kiasi cha kutupiwa lawama waamuzi lile bao la Kagere alilofunga kwa penalti baada ya video kuonyesha hakuwa ameshikwa na Kelvin Yondan ndani ya boksi kama ambavyo Jonesia alitafsiri.

Tukio lingine ni lile la beki wa Simba, Pascal Wawa kumfanyia madhambi ya makusudi Ditram Nchimbi kwa kumkanyanga kiasi cha kushindwa kuendelea na mchezo lakini lilishindwa kutolewa adhabu.

Wakati huo huo, Bodi ya Ligi imetoa onyo kwa mwamuzi Florentina Zabron aliyechezesha mchezo namba 17 kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga katika uwanja wa Sokoine uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.

Kwa mujibu wa Kamati ya saa 72, Florentina aliamuru mchezo kuchezwa katika uwanja ambao hakuwa kwenye hali nzuri kutokana na mvua lakini pia alionekana kushindwa kutafsiri vizuri sheria 17 za soka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles